Taarifa Namba 1 kutoka Makao Makuu ya Majeshi ya Iran
(last modified Fri, 13 Jun 2025 04:15:51 GMT )
Jun 13, 2025 04:15 UTC
  • Taarifa Namba 1 kutoka Makao Makuu ya Majeshi ya Iran

Kitengo cha Mawasiliano cha Makao Makuu ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kimetoa taarifa rasmi kikilaani vikali uvamizi wa wazi uliofanywa na adui muovu wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la IRIB, mashambulizi ya kichokozi na ya uvamizi yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni alfajiri ya Ijumaa, tarehe 13 Juni, yamelenga maeneo ya kijeshi na yasiyo ya kijeshi ndani ya Iran, na yamesababisha mashahidi na majeruhi miongoni mwa raia, wakiwemo wanawake, watoto, na baadhi ya makamanda wa vikosi vya ulinzi vya taifa.

Makao Makuu ya Majeshi, sambamba na kulaani vikali ukiukaji huu wa wazi wa sheria na kanuni zote za kimataifa, na kwa mujibu wa agizo la Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi wa Iran (roho yake idumu), yanawahakikishia wananchi mashujaa, wacha Mungu na waumini wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa:

Majibu ya wanajeshi wenu dhidi ya walioamuru, waliotekeleza, na wale wanaosaidia jinai hii ya kusaliti, yatakuwa ya kushtua, makali, na ya kuwaacha wakijutia uamuzi wao.