IRGC: Iran itatoa majibu madhubuti kwa chokochoko mpya za maadui
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i131078-irgc_iran_itatoa_majibu_madhubuti_kwa_chokochoko_mpya_za_maadui
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limewaonya maadui wa Iran hususan Israel na Marekani kwamba, watakabiliwa na majibu makali na madhubuti ya Jamhuri ya Kiislamu iwapo watafanya makosa yoyote mapya au kufanya kitendo chochote cha uchokozi dhidi ya nchi hii.
(last modified 2025-09-22T04:24:37+00:00 )
Sep 21, 2025 11:06 UTC
  • IRGC: Iran itatoa majibu madhubuti kwa chokochoko mpya za maadui

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limewaonya maadui wa Iran hususan Israel na Marekani kwamba, watakabiliwa na majibu makali na madhubuti ya Jamhuri ya Kiislamu iwapo watafanya makosa yoyote mapya au kufanya kitendo chochote cha uchokozi dhidi ya nchi hii.

IRGC imetoa indhari hiyo leo Jumapili katika taarifa yake iliyotolewa kwa mnasaba wa kuanza Wiki ya Kujihami Kukatifu, ambayo ni kumbukumbu ya kuanza kwa vita vya miaka minane vya utawala uliopinduliwa wa dikteta wa Iraq, Saddam Hussein dhidi ya Iran katika miaka ya 1980.

Taarifa ya SEPAH imesema: Iran ililinda ardhi na mamlaka yake ya kujitawala kwa kutegemea uungwaji mkono wa wananchi, huku utawala wa Saddam ukipata uungwaji mkono wa kifedha na kijeshi kutoka nchi za Magharibi. 

"Wiki ya Kujihami Kutakatifu, kwa kweli, ni sherehe ya ushindi wa mapmabano ya wananchi wazalendo, ikikumbusha moja ya kipengee cha kuvuatia zaidi katika historia ya Mapinduzi ya Kiislamu. Ni chanzo cha fahari ya kitaifa, na chache ya Muqawama katika anga za kimataifa," imesema taarifa hiyo.

Huku ikisisitiza kwamba Marekani na Israel zilishindwa kufikia "malengo yao ya kishetani na ovu" katika vita vya siku 12 dhidi ya Iran mwezi Juni mwaka huu, IRGC imesema kwamba, vikosi vyake pamoja na vikosi vingine vya kijeshi vya Iran vinaendelea kuimarisha uwezo wao wa kivita pamoja na nguvu za kushambulia na kujihami, na uwezo wa kimkakati siku baada ya siku.

Wanajeshi wa SEPAH

Kabla ya hapo, Waziri wa Ulinzi wa Iran, Brigedia Jenerali Aziz Nasirzadeh alisisitiza kuwa, iwapo maadui watafanya uchokozi mwingine dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, bila shaka majeshi ya nchi hii yatatumia vifaa, silaha na zana za kijeshi ambazo hazijawahi kutumiwa kufikia sasa dhidi ya maadui.

Wakati huo huo, Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu Iran, Meja Jenerali Amir Hatami amesisitiza kuwa Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu vimejiweka tayari kutoa jibu kwa wavamizi ambalo ni la "kusagasaga zaidi" kuliko lile lililoonekana wakati wa uchokozi uliofanywa na utawala haramu wa kizayuni wa Israel na Marekani dhidi ya taifa hili.