Iran yaidhinisha miradi ya uwekezaji wa kigeni ya dola milioni 485
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i133526-iran_yaidhinisha_miradi_ya_uwekezaji_wa_kigeni_ya_dola_milioni_485
Bodi ya uwekezaji wa kigeni ya Iran imeidhinisha maombi 67 yenye thamani ya dola milioni 485 wakati wa mkutano wake wa tisa wa mwaka, kuashiria maslahi mapya kutoka kwa wawekezaji wa kimataifa katika sekta nyingi.
(last modified 2025-11-24T05:35:48+00:00 )
Nov 24, 2025 03:03 UTC
  • Iran yaidhinisha miradi ya uwekezaji wa kigeni ya dola milioni 485
    Iran yaidhinisha miradi ya uwekezaji wa kigeni ya dola milioni 485

Bodi ya uwekezaji wa kigeni ya Iran imeidhinisha maombi 67 yenye thamani ya dola milioni 485 wakati wa mkutano wake wa tisa wa mwaka, kuashiria maslahi mapya kutoka kwa wawekezaji wa kimataifa katika sekta nyingi.

Uidhinishaji wa hivi majuzi unasisitiza juhudi za Iran kuvutia uwekezaji wa kigeni licha ya vikwazo vinavyoendelea na kutokuwa na uhakika wa kikanda. Kwa kuwekeza katika sekta mbalimbali na kushirikiana na washirika kutoka Asia, Ulaya na Asia Magharibi, Tehran inalenga kuimarisha uthabiti wa kiuchumi na kupanua ushirikiano wa kimataifa.

Mkutano huo, ulioongozwa na Mehdi Heidari, Kaimu Mkuu wa Shirika la Uwekezaji, Misaada ya Kiuchumi na Kiufundi la Iran, ulifanyika katika mji wa Tabriz ulioko kaskazini magharibi mwa Iran.

Kati ya maombi 73 ya uwekezaji yaliyopitiwa, 67 yaliidhinishwa, yakijumuisha sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na viwanda, ujenzi wa mitambo ya kusafisha mafuta, nishati mbadala, magari, madini, dawa, afya, usafirishaji na huduma.

Nchi zinazohusika katika miradi hiyo ya uwekezaji iliyoidhinishwa ni Umoja wa Falme za Kiarabu, Uchina, Ujerumani, Uturuki, India, Georgia, Afghanistan, Pakistan, pamoja na Wairani wanaoishi nje ya nchi.

Wajumbe wa bodi walitembelea miradi iliyofanikiwa ya uwekezaji wa kigeni katika Mkoa wa Azabajan Mashariki na kukutana moja kwa moja na wawekezaji. Walijitolea kushughulikia changamoto zilizoko na kutoa masuluhisho ili kurahisisha utendakazi.

Hayo yanaripotiwa huku Iran ikifanya vyema katika uuzaji wa bidhaa zake nje ya nje huusuusan barani Afrika.

Mauzo ya bidhaa za Iran barani Afrika yaliongezeka maradufu katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu (1404 Hijria Shamsia), na kufikia dola milioni 675.