Danny Citrinowicz: Ushawishi wa vyombo vya habari vya Iran barani Afrika umeongezeka
-
Danny Citrinowicz: Ushawishi wa vyombo vya habari vya Iran barani Afrika umeongezeka
Mtafiti mkuu wa Mpango wa Iran katika Taasisi ya Utafiti wa Usalama wa Taifa ya Israel (INSS) ameeleza wasiwasi wake kuhusu mwenendo wa ushawishi wa vyombo vya habari vya Iran barani Afrika na matokeo yake ya muda mrefu dhidi ya maslahi ya utawala wa Kizayuni barani humo.
Katika Podikasti ya Kiebrania "Confidence" Danny Citrinowicz ameelezea hali mbalimbali za uwepo wa Iran barani Afrika, na kusema kuwa katika miaka ya hivi karibuni, Iran imeanzisha mfumo mpana wa vyombo vya habari barani Afrika, unaojumuisha kutangaza mitandao ya Kiiran katika lugha mbalimbali, zikiwemo lugha za ndani za Kiafrika.
Danny Citrinowicz alitaja chaneli kadhaa maalum za Irani katika muktadha huu kama Press TV, Al-Alam, Hispan TV na Hausa TV.
Kwa mujibu wake, kanali hizi ni sehemu ya utaratibu wa ushawishi wa Iran katika jamii mbalimbali za Kiafrika; utaratibu unaochanganyika na vituo vya kidini vya Kiislamu, taasisi za kitamaduni, mitandao ya kijamii, na shughuli za Hilali Nyekundu ya Iran, kutoa msingi wa kuunda ushawishi wa kijamii na kisiasa.
Mtaalamu huyo wa Israel alisema kuwa Iran imeweza kushawishi jamii za Kishia na sehemu za maoni ya wananchi katika nchi kama vile Nigeria, Ivory Coast na Senegal kupitia mifumo hii; shughuli ambazo, alikiri, katika baadhi ya kesi zimesababisha uhamasishaji mitaani na kushawishi maamuzi ya serikali.
Kwa mujibu wa mtaalamu huyo wa Israel, sehemu kubwa ya shughuli za Iran barani Afrika inatekelezwa kwa njia ya nguvu laini na kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kiutamaduni na kidini; eneo ambalo, kulingana naye, serikali nyingi za Kiafrika hata hazifahamu undani wake wa kweli.