Spika Qalibaf: Marekani ina chuki ya kihistoria na mwanachuo wa Kiirani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i134022-spika_qalibaf_marekani_ina_chuki_ya_kihistoria_na_mwanachuo_wa_kiirani
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa: Mfumo wa kibeberu kinara wake akiwa Marekani una chuki na uadui wa kihistoria dhidi ya mwanachuo wa Kiirani.
(last modified 2025-12-07T06:52:47+00:00 )
Dec 07, 2025 06:52 UTC
  • Spika Qalibaf: Marekani ina chuki ya kihistoria na mwanachuo wa Kiirani

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa: Mfumo wa kibeberu kinara wake akiwa Marekani una chuki na uadui wa kihistoria dhidi ya mwanachuo wa Kiirani.

Mohammad Baqer Qalibaf amesema hayo leo katika kikao cha Bunge na kubainisha kwamba, "Kwanza kabisa, napenda kuwapongeza wanachuo wote wapendwa kwa kuwadia tarehe 16 Azar (Disemba 7) ambayo ni Siku ya Mwanachuo."

Spika Qalibaf amesema, Amesema: "Wanachuo katika historia ya zama hizi ya Iran wamekuwa mstari wa mbele na viongozi wa kijamii katika vita dhidi ya mabeberu na madhalimu, na katika suala hili, sio tu hawakuwa waigaji wengine, bali wao wenyewe walionyesha njia kwa wanajamii wengine."

Spika wa Bunge la Iran ameeleza kuwa, mfumo wa kibeberu unaoongozwa na Marekani, una chuki na uadui wa kihistoria dhidi ya mwanachuo wa Kiirani kwa sababu mwanachuo wa Kiirani alisimama peke yake dhidi ya uporaji wao, akajilinda, na akauawa shahidi ili taifa la Iran lipate ufahamu wa kihistoria kwamba demokrasia na maendeleo hayataepuka kutoka kwenye bomba la bunduki la mfumo wa kibeberu.

Jumapili ya leo tarehe 16 Azar inasadifiana na tarehe 7 Disemba ambapo mwaka 1953 wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Iran walifanya maandamano mbele ya Chuo Kikuu cha Tehran kulaani na kulalamikia ziara ya Richard Nixon, makamu wa rais wa wakati huo wa Marekani na uingiliaji wa Washington katika masuala ya ndani ya Iran.

Maandamano hayo ya wanachuo yalikandamizwa na utawala kibaraka wa Pahlavi. Wanajeshi wa utawala huo wa kidikteta wa Shah waliua wanachuo watatu na kujeruhi mamia ya wengine kwenye maandamano ya siku hiyo. Siku hii inajulikana katika kalenda ya matukio ya Jamhuri ya Kiislamu kuwa Siku ya Mwanachuo.