Marekani inahusika katika kugeuza maandamano ya amani kuwa machafuko nchini Iran
Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Bw. Amir-Saeid Iravani katika Umoja wa Mataifa ameliandikia barua Baraza la Usalama la umoja huo akisema Marekani imeyageuza malalamiko na maandamano ya amani ya wananchi wa Iran kuwa ghasia na machafuko.
Balozi Iravani amelaani mienendo inayokiuka sheria ya Marekani na ushirikiano wake na utawala wa Kizayuni wa Israel katika kuingilia mambo ya ndani ya Iran. Amesema uingiliaji kati huo unafanyika kwa kutumia vitisho, uchochezi wa machafuko na kuvuruga amani na utulivu.
Balozi Iravani amelaani mienendo inayokiuka sheria ya Marekani na ushirikiano wake na utawala wa Kizayuni wa Israel katika kuingilia mambo ya ndani ya Iran. Amesema uingiliaji kati huo unafanyika kwa kutumia vitisho, uchochezi wa machafuko na kuvuruga amani na utulivu.
Balozi wa Iran Umoja wa Mataifa amesisitiza akisema: Tunalaani vitendo hivyo vinavyovuruga amani na kinyume na Hati ya Umoja wa Mataifa.
Awali, Baraza la Usalama wa Taifa la Iran lilikuwa limetoa taarifa, -ambayo mbali na kuashiria kuwa tangu baada ya vita vya siku 12 Marekani na utawala wa kizayuni wa Israel hazijaacha kufanya chokochoko za vita na uadui dhidi ya taifa la Iran-, imesisitiza kwamba: taifa linaloheshimika la Iran litazivunja mbinu za kihujuma na kufanya uharibifu za adui kwa umoja na mshikamano wa kitaifa.
Sehemu moja ya taarifa hiyo imesema: Wakati wa vita vya siku 12 na mpaka leo utawala wa kizayuni wa Israel unaendelea kufanya dhulma dhidi ya Wairani kupitia vita mseto, na unabadilisha mbinu baadhi ya wakati. Hata hivyo, haujaacha chokochoko za vita dhidi ya taifa lisilorudi nyuma la Iran, ambapo matukio ya karibuni, japokuwa yalianza kwa kulalamikia kuvurugika kwa soko la uchumi, lakini yameibua machafuko nchini kwa uongozi na ubunifu wa adui mzayuni.
Taarifa hiyo ya Baraza la Usalama wa Taifa la Iran imeendelea kueleza: Matamshi aliyotoa Trump katika siku zilizopita yanadhihirisha kuwepo mpango wa pamoja uliofanywa na tawala hizo mbili ambao unayafanya maisha ya wananchi wa Iran yasiwe na amani.
Sisitizo la Iran kuhusu kuhusika moja kwa moja Marekani na Israel katika ghasia na fujo na kuchochea magenge ya wanaotekeleza uharibifu nchini Iran linaweza kufahamika kwa kuzingatia mienendo na matamshi ya Rais Donald Trump wa Marekani na Benjamin Netanyahu, waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
Katika siku za hivi karibuni, mbali na kuwa Trump ametangaza kuunga mkono magenge yanayoibua fujo nchini Iran, amesema atakabiliana na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu iwapo kutachukuliwa hatua za kukabiliana na magenge ya wanaoibua fujo. Inaelekea kuwa, lengo kuu la Trump katika matamshi yake ya hivi karibuni ya vitisho dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kuwachochea zaidi wanaoibua fujo ili waendeleze ugaidi, ghasia na uharibufu. Netanyahu naye pia ametangaza mara kadhaa kuwa anaunga mkono magenge ya wahalifu na magaidi nchini Iran.
Ni wazi kuwa rais Trump wa Marekani amelisababishia taifa la Iran hasara kubwa kwa sera zake za mashinikizo ya juu kabisa kupitia vikwazo vya upande mmoja na kisha kwa kushirikiana na utawala haramu wa Israel katika kushambulia vituo vya nyuklia vya Iran katika vita vya siku 12 mwezi juni mwa jana. Pamoja na hayo anajitokeza na kudai kuwa eti anawaunga mkono wananchi wa Iran.
Katika duru yake ya kwanza ya urais na pia katika duru hii ya pili ameshadidisha sera ya 'mashinikizo ya juu kabisa' dhidi ya Iran lengo likuwa ni kuhakikisha Iran haiuzi mafuta ili hatimaye isalimu amri mbele ya matakwa ya Washington katika uga wa nyukia, makombora na sera za kieneo.
Sera hizi za vikwazo hazilengi tu serikali bali zimewaathiri wananchi katika mahitaji yao ya kila siku ikiwa ni pamoja na kushuka kwa kiasi kikubwa kwa thamani ya sarafu ya Rial ya Iran. Ni vipi mtu ambaye ametekelelza sera hizo ambazo hata zimewazuia Wairani kupata baadhi ya dawa muhimu sasa anadai kuwa anawajali wananchi wa Iran.?
Matamshi ya hivi karibuni ya Rais wa Marekani ya eti kuonyesha kuwajali wananchi wa Iran yanapaswa kuchunguzwa kwa kuzingatia sera za huko nyuma za uhasama za watawala wa Washington dhidi ya Iran.
Trump ambaye katika muda wote wa uongozi wake anazungumza kuhusu mashinikizo na vikwazo vya kisiasa na kiuchumi na hata kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya taifa la Iran leo anadai kuunga mkono taifa hilo hilo. Ni wazi kuwa kuna mgongano wa wazi katika sera hizo ambazo kimsingi lengo lake kuu ni uhasama na chuki dhidi ya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Inavyoelekea ni kuwa lengo la Trump katika matamshi ya kuwaunga mkono magaidi wanaoibua ghasia Iran ni kushadidisha vita vya kisaikolojia ili kufikia malengo yake ya vikwazo na vitisho vya kijeshi dhidi ya Iran.