Jeshi la Iran laionya Israel kuhusu ukiukaji usitishaji vita Lebanon
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i139222-jeshi_la_iran_laionya_israel_kuhusu_ukiukaji_usitishaji_vita_lebanon
Kamandi Kuu ya Majeshi ya Iran, Khatam al-Anbiya imeuonya utawala wa Israel na kuutaka usitishe mara moja ukiukaji wa mara kwa mara wa makubaliiano ya usitishaji vita kusini mwa Lebanon, au ukabiliwe na “jibu kali” la majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
(last modified 2026-07-03T11:45:53+00:00 )
Jun 17, 2026 12:10 UTC
  • Eneo la Lebanon na Nabatieh liliwa chini ya mashambulizi ya Israel
    Eneo la Lebanon na Nabatieh liliwa chini ya mashambulizi ya Israel

Kamandi Kuu ya Majeshi ya Iran, Khatam al-Anbiya imeuonya utawala wa Israel na kuutaka usitishe mara moja ukiukaji wa mara kwa mara wa makubaliiano ya usitishaji vita kusini mwa Lebanon, au ukabiliwe na “jibu kali” la majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Katika taarifa yake, kamandi hiyo imesema kuwa “jeshi la kigaidi la utawala wa Kizayuni” limekiuka usitishaji vita mara 84 katika kipindi cha siku mbili licha ya tangazo la Rais wa Marekani kuhusu kuhitimishwa vita hivyo.

Taarifa hiyo imesema: “Ikiwa jeshi hilo katili la utawala wa Kizayuni halitakomesha vitendo vyake viovu kusini mwa Lebanon, litakumbana na jibu kali kutoka kwa majeshi madhubuti ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran."

Onyo hili la Iran limetolewa baada ya kutangazwa mkataba wa maelewano (MoU) kati ya Tehran na Washington, ambao unalenga kuhitimisha vita dhidi ya Iran..

Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema kuwa shambulio lolote la Israel dhidi ya Lebanon au kuendelea kukalia kwa mabavu maeneo yaliyotekwa hivi karibuni katika nchi hiyo ya Kiarabu, kutatambuliwa kama ukiukwaji wa mkataba wa maelewano (MoU) unaotarajiwa kusainiwa kati ya Iran na Marekani.

Akizungumza katika mkutano na wanadiplomasia wa kigeni jijini Tehran siku ya Jumanne, Araghchi alibainisha kuwa nguzo kuu ya mkataba huo ni tamko la kusitisha vita mara moja na kwa kudumu katika nyanja zote, ikiwemo Lebanon.

Hivyo basi, alisisitiza kuwa kukomeshwa kwa uchokozi dhidi ya Lebanon ni sehemu muhimu na isiyotenganishika ya mkataba huo.

Katika kipindi cha vita vya kichokozi vya Marekani na Israel, dhidi ya Iran ambavyo vilianza Februari 28 hadi Aprili 7, majeshi ya Iran yalifanya operesheni za kulipiza kisasi dhidi ya ngome za tawala hizo mbili. Iran pia ilijibu uchokozi wa Israel dhidi ya Lebanon.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ilisema Jumapili kuwa mkataba huo wa maelewano umekamilika na utatiwa saini rasmi nchini Uswisi siku ya Ijumaa. Chini ya makubaliano hayo, vita katika nyanja zote, ikiwemo Lebanon, vitakomeshwa.