Iran ndiyo nguvu mpya ya kikanda, si Marekani au 'Israel': The Atlantic
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i140930-iran_ndiyo_nguvu_mpya_ya_kikanda_si_marekani_au_'israel'_the_atlantic
Mtaalamu maarufu wa masuala ya kimikakati wa kihafidhina wa Marekani amesema kwamba vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran vimekuwa na matokeo kinyume na matarajio, na vimeshindwa kuilazimisha Tehran kusalimu amri, na badala yake vimeimarisha ushawishi wa Iran wa kikanda, vikifichua mipaka ya nguvu za kijeshi za Marekani na kugeuza Lango-Bahari la Hormuz kuwa chanzo kikuu cha ushawishi wa Jamhuri ya Kiislamu.
(last modified 2026-08-24T13:48:41+00:00 )
Aug 24, 2026 13:43 UTC
  • Iran ndiyo nguvu mpya ya kikanda
    Iran ndiyo nguvu mpya ya kikanda

Mtaalamu maarufu wa masuala ya kimikakati wa kihafidhina wa Marekani amesema kwamba vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran vimekuwa na matokeo kinyume na matarajio, na vimeshindwa kuilazimisha Tehran kusalimu amri, na badala yake vimeimarisha ushawishi wa Iran wa kikanda, vikifichua mipaka ya nguvu za kijeshi za Marekani na kugeuza Lango-Bahari la Hormuz kuwa chanzo kikuu cha ushawishi wa Jamhuri ya Kiislamu.

Akiandika katika The Atlantic chini ya kichwa “Iran Unleashed,” Robert Kagan anasema kwamba mlingano wa nguvu katika Asia Magharibi umebadilika sana baada ya Iran kusimama kidete dhidi ya mashambulizi ya mara kwa mara ya Marekani na Israel bila kukubali matakwa ya Washington.

Kwa kuzingatia historia yake ya kisiasa, tathmini hiyo ya mhafidhina mambo leo wa Marekani inaashiria kukiri kwa kushangaza kushindwa mkakati wa vita wa Washington dhidi ya Iran. Pia inakiri kuwa Iran ilipata ushindi wa kimkakati na kwamba Tehran imeibuka kidedea kwenye kampeni hiyo bila ya kujisalimisha, na kujijengea ngome, ushawishi na nguvu kubwa zaidi kuliko kabla ya vita.

Kagan anaandika: "Nguvu kuu katika eneo la Magharibi mwa Asia siku zijazo itakuwa Iran, si Marekani au Israel" akisema kwamba mataifa jirani tayari yanazoea mazingira ya kikanda yaliyobadilika kimsingi.

Robert Kagan ameyataja makubaliano ya Juni 2026 kati ya Iran na Marekani yaliyosimamiwa na Pakistan kuwa yanaakisi mlingano huo mpya wa nguvu. Chini ya makubaliano hayo, Iran "ingesimamia mipango ya safari na kupitisha salama meli za kibiashara katika Lango Bahari la Hormuz", huku Tehran na Oman zikijadili usimamizi wa lango hilo "kwa mujibu na sheria ya kimataifa inayotumika na haki za mamlaka ya nchi za pwani."

Ameyataja makubaliano hayo kuwa ni faida kubwa kwa Iran, akisema kwamba hayakurejesha utaratibu wa safari za baharini wa kabla ya vita wala hayakuipa Washington jukumu lolote la kusimamia njia hiyo muhimu ya majini.

Kagan pia ameashiria uhaba wa makombora na zana muhimu za kivita za Marekani katika vita vyake dhidi ya Iran, akisema kwamba kampeni nyingine ndefu ya vita dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ingedhoofisha utayarifu wa Marekani kwingineko, ikiwa ni pamoja na katika makabiliano yanayoweza kutokea baina ya nchi hiyo na China au Russia.