Magaidi wanaopata msaada wa Saudia wauawa nchini Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i15163-magaidi_wanaopata_msaada_wa_saudia_wauawa_nchini_iran
Askari wa Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) wamesambaratisha mtandao wa magaidi wanaopata himaya ya Saudi Arabia na Marekani katika mkoa wa Sistan na Baluchestan kusini mashariki mwa nchi.
(last modified 2026-03-27T07:58:19+00:00 )
Sep 12, 2016 03:31 UTC
  • Magaidi wanaopata msaada wa Saudia wauawa nchini Iran

Askari wa Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) wamesambaratisha mtandao wa magaidi wanaopata himaya ya Saudi Arabia na Marekani katika mkoa wa Sistan na Baluchestan kusini mashariki mwa nchi.

Taarifa iliyotolewa Jumapili usiku imebaini kuwa, askari wa IRGC walikabiliana na wanachama kadhaa wa kundi la kigaidi linalojiita Jaish ul-Adl katika eneo la Kouhak karibu na mpaka wa Pakistan siku chache zilizopita ambapo magaidi watano waliangamizwa.

Karika oparesheni hiyo, maafisa wa usalama pia walifanikiwa kunasa idadi kubwa ya silaha, vifaa vya mawasiliano, kamera za kutumika usiku na magari matatu yaliyokuwa yakitumiwa na magaidi walioangamizwa.

Askari wa kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC

 

Kundi la kigaidi linalojiita Jaish ul- Adl limehusika na mauaji ya raia wengi na pia askari wa mpakani nchini Iran.

Jaish ul Adl ni kijikundi cha magaidi wa Kiwahhabi wanaopata misaada ya kifedha kutoka Saudia na linaendesha oparesheni zake za kigaidi dhidi ya Iran katika eneo la mpakani nchini Pakistan.