Kazem Jalali: Sera za Iran zinalenga kuleta umoja katika Umma wa Kiislamu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i17707-kazem_jalali_sera_za_iran_zinalenga_kuleta_umoja_katika_umma_wa_kiislamu
Mjumbe wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Sera za Nje ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesema sera za kieneo na kimataifa za Iran ziko wazi kabisa na zinalenga kuleta umoja katika Umma wa Kiislamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 19, 2016 00:33 UTC
  • Kazem Jalali: Sera za Iran zinalenga kuleta umoja katika Umma wa Kiislamu

Mjumbe wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Sera za Nje ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesema sera za kieneo na kimataifa za Iran ziko wazi kabisa na zinalenga kuleta umoja katika Umma wa Kiislamu.

Kazem Jalali ameyasema hayo wakati akihutubia kikao cha 36 cha kamati ya utendaji ya Umoja wa Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kilichofanyika jana mjini Ankara,Uturuki.

Amesema kuimarisha uhusiano baina ya nchi za Kiislamu hususan nchi jirani ni kipaumbele kikuu cha sera za nje za Iran.

Mkutano wa 13 wa viongozi wa OIC, Uturuki

Mjumbe wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Sera za Nje ya Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa Jamhuri ya Kiislamu inaitakidi kwamba kutatua kwa njia ya amani tofauti na sutafahamu zinazojitokeza kunawezekana tu kwa mazungumzo na njia za kidiplomasia.

Jalali amekumbusha pia harakati za makundi ya kigaidi katika eneo la Mashariki ya Kati na kubainisha kwamba harakati kubwa na zinazoshamiri za makundi ya kigaidi na yenye misimamo ya kufurutu mpaka katika eneo hili hasasi na muhimu si tishio kubwa kwa amani na uthabiti wa nchi za eneo hili pekee bali ni changamoto kwa jamii nzima ya kimataifa.

Magaidi wa kundi la Daesh wanaotenda kila aina ya jinai

Kazem Jalali, ambaye pia ni mkuu wa kituo cha utafiti cha bunge la Iran aidha ameashiria harakati za kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh katika nchi za Iraq na Syria na kusisitiza kuwa nchi zote za Kiislamu zina wajibu wa kuzisaidia na kuziunga mkono serikali za nchi hizo katika kupambana na kundi hilo.

Kuhusu hali mbaya na ya kusikitisha ya Yemen, mjumbe wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Sera za Nje ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema nchi hiyo imefikia hatua na marhala hatari sana kutokana na kuuawa na kujeruhiwa maelfu ya watu na kuteketezwa miundombinu yake.../