Iran yakanusha kuhusika na shambulio dhidi ya manowari za Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i17797-iran_yakanusha_kuhusika_na_shambulio_dhidi_ya_manowari_za_marekani
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekanusha vikali madai ya jenerali wa jeshi la Marekani kwamba kuna uwezekano wa kuhusika Tehran katika shambulio la kombora dhidi ya manowari ya nchi hiyo Bahari Nyekundu.
(last modified 2026-09-20T16:32:32+00:00 )
Oct 20, 2016 04:19 UTC
  • Iran yakanusha kuhusika na shambulio dhidi ya manowari za Marekani

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekanusha vikali madai ya jenerali wa jeshi la Marekani kwamba kuna uwezekano wa kuhusika Tehran katika shambulio la kombora dhidi ya manowari ya nchi hiyo Bahari Nyekundu.

Mbali na kuyaelezea madai hayo ya Jenerali wa jeshi la Marekani Joseph Votel kuwa ni ya kutia shaka na yasiyo na msingi, Bahram Qassimi amesisitiza kuwa matamshi hayo ni kisa cha kubuni kilichochanganyika na dhana mbaya inayotokana na kuchanganyikiwa Marekani.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameongeza kuwa serikali ya Marekani inapaswa ijihadhari na hatua za watu ambao wanatapatapa ndani ya lindi la kinamasi cha vita vya Yemen kutokana na uvamizi wao wa kinyama waliofanya dhidi ya nchi hiyo na ambao wanataka kujiokoa na fedheha ya kushindwa katika vita hivyo kwa kushadidisha mivutano na kupanua wigo wa vita na machafuko ili kuwatumbukiza na wengine pia kwenye vita vya Yemen visivyo na tija.

Image Caption

Bahram Qassimi amebainisha kuwa wanajeshi wa Marekani, ambao hawawezi kukanusha kuhusika kwao katika jinai dhidi ya wananchi wa Yemen kutokana na kuusaidia moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia katika jinai hizo, badala ya kutaka kujipapatua na kutaka kuelekeza lawama kwa wengine wazuie umwagaji damu zaidi na kukomesha mauaji yanayofanywa na washirika wao dhidi ya raia madhulumu na wasio na ulinzi wa Yemen.../