Iran: Uungaji mkono wa Saudia kwa ugaidi umelitumbukiza eneo kwenye machafuko
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i23041-iran_uungaji_mkono_wa_saudia_kwa_ugaidi_umelitumbukiza_eneo_kwenye_machafuko
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema Saudi Arabia imelitumbukiza eneo la Mashariki ya Kati kwenye machafuko kwa kuyaunga mkono makundi ya kitakfiri na kigaidi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 08, 2017 00:12 UTC
  • Iran: Uungaji mkono wa Saudia kwa ugaidi umelitumbukiza eneo kwenye machafuko

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema Saudi Arabia imelitumbukiza eneo la Mashariki ya Kati kwenye machafuko kwa kuyaunga mkono makundi ya kitakfiri na kigaidi.

Bahram Qassemi ameyasema hayo kujibu matamshi yaliyotolewa na Waziri wa Ulinzi na kaimu mrithi wa Ufalme wa Saudia dhidi ya Iran.

Amesema, miongoni mwa wadau ambao inawalazimu warekebishe mwenendo wao kwa ajili ya utulivu na amani ya dunia ni Saudi Arabia.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, hakuna shaka yoyote kuwa ugaidi wa kitakfiri chimbuko lake linatokana na fikra ya Uwahabi na kuongeza kwamba Saudi Arabia, kwa upande mmoja ni msababishaji wa jinai za umwagaji damu dhidi ya wananchi wa Syria, Iraq na Yemen; na kwa upande mwingine, kutokana na kushirikiana na kuwa kitu kimoja na utawala wa Kizayuni wa Israel imewafanyia jinai Waislamu hususan Ulimwengu wa Kiarabu na malengo matukufu ya Palestina.

Magaidi wa kundi la kitakfiri la Daesh lenye fikra za Kiwahabi na linaloungwa mkono na Saudia

Bahram Qassemi amesisitiza kuwa ripoti za mashirika ya intelijinsia ya Magharibi zimethibitisha mara kadha wa kadha kuwepo uhusiano wa maana maalumu na ulioratibiwa baina ya vyombo rasmi vya Saudia na watu wenye misimamo ya kufurutu mpaka ya kitakfiri duniani kote; hivyo inavyoonekana, matamshi ya Waziri wa Ulinzi wa Saudia ni aina fulani ya kujipapatua na kujitoa kimasomaso kutokana na ufichuaji huo wa taarifa za kiintelijinsia.

Muhammad bin Salman, Waziri wa Ulinzi wa Saudia

Muhammad bin Salman, Waziri wa Ulinzi na kaimu mrithi wa Ufalme wa Saudi Arabia amedai katika mahojiano aliyofanyiwa na jarida la Foreign Policy la Marekani kwamba Iran ni mwakilishi wa mambo matatu makuu; yaani idiolojia zisizo na mipaka, kuvuruga uthabiti na ugaidi.../