Jan 09, 2017 04:33 UTC
  • Iran yatahadahrisha kuhusu njama za kuvuruga mchakato wa amani Syria

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeonya kuhusu njama za kuvuruga mchakato mgumu wa kusaka amani nchini Syria.

Admeli Ali Shamkhani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ameyasema hayo Jumapili mjini Damascus wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Bashar al Assad wan chi hiyo.

Amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina azma ya kusaidia kutekelewaji wa mchakato wa kisiasa kwa lengo la kumaliza vita vya ndani ambavyo vinakaribia mwaka wa sita sasa.

Amesema mazumgumzo ya kisiasa yanapaswa kufanyika baina ya Wasyria wenyewe na wenyewe waongoze mazungumzo hayo na kazi ya Umoja wa Mataifa na nchi zenye ushawishi Syria iwe ni kuratibu tu mazungumzo hayo. 

Shamkhani na Rais Assad

Amesema kuna haja ya kuhakikisha kunafanyika juhudi za pamoja za mazungumzo huko Damascus kama mji mkuu wa Syria iliyoungana.

Shamkhani ambaye pia ni msimamizi wa masuala ya kisiasa, kiusalama na kiulinzi baina ya Iran, Russia na Syria ameongeza kuwa, mrengo wa vita dhidi ya ugaidi hivi sasa umepata msukumo kutokana na ushirikiano uliopo baina ya Tehran, Damascus na Moscow.

Aidha amempongeza Rais Assad kwa nafasi yake ya kuongoza serikali na majeshi ya Syria katika vita dhidi ya magaidi wakufurishaji jambo ambalo limepelekea kupatikane mafanikio makubwa.

 

Tags