Filamu ya Forushande yashinda tuzo ya Oscar
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i25688-filamu_ya_forushande_yashinda_tuzo_ya_oscar
Filamu ya Forushande (The Salesman) iliyotengenezwa na Asghar Farhadi imeshinda tuzo ya Oscar katika kitengo cha filamu za kigeni kwenye Academia ya Filamu ya Marekani.
(last modified 2026-08-17T09:53:57+00:00 )
Feb 27, 2017 01:19 UTC
  • Filamu ya Forushande yashinda tuzo ya Oscar

Filamu ya Forushande (The Salesman) iliyotengenezwa na Asghar Farhadi imeshinda tuzo ya Oscar katika kitengo cha filamu za kigeni kwenye Academia ya Filamu ya Marekani.

Filamu hiyo ya Forushande ilikuwa imewekwa katika orodha ya filamu tano za kigeni za sherehe ya 89 za Academia ya Oscar. 

Hii ni mara ya pili kwa mtengeneza filamu, Asghar Farhadi wa Iran kushinda tuzo ya filamu ya Oscar. Mwaka 2012 pia Asghar Farhadi alishinda tuzo hiyo kwa filamu ya "A Separation".

Hata hivyo Farhadi na wachezaji wote katika filamu ya The Salesman hawakushirika katika hafla ya tuzo ya filamu ya Oscar huko Marekani iliyofanyika mapema leo kwa wakati wa Tehran wakilalamika na kuonesha upinzani wao dhidi ya amri ya Rais wa nchi hiyo, Donald Trump inayowapiga marufuku raia wa nchi za Waislamu kuingia Marekani.

Taarifa ya Asghar Farhadi iliyosomwa na mwanahewa wa kwanza Muirani kwenda katika anga za mbali, Anushe Ansari imesema: Kutoshiriki kwake katika sherehe za Oscar ni kwa ajili ya kuonesha heshima kwa taifa la Iran na nchi nyingine sita za Kiislamu ambao wamevunjiwa heshika kwa sheria isiyo ya kibinadamu inayowazuia wahajiri kuingia Marekani.