Kuimarishwa uhusiano wa Iran na Kodivaa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i2893-kuimarishwa_uhusiano_wa_iran_na_kodivaa
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa tayari kuimarisha uhusiano wake na Ivory Coast katika nyanja mbali mbali.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 12, 2016 04:32 UTC
  • Kuimarishwa uhusiano wa Iran na Kodivaa

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa tayari kuimarisha uhusiano wake na Ivory Coast katika nyanja mbali mbali.

Hussein Mulla Abdullahi Mkurugenzi Mkuu wa Afrika Katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameyasema hayo katika mkutano na Abdullah Mabri Waziri wa Mambo ya Nje wa Ivory Coast mjini Abdijan mji mkuu wa nchi hiyo. Sambamba na kumkabidhi ujumbe wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, pia amesema Iran iko tayari kuimarisha uhusiano na nchi hiyo katika nyanja mbali mbali.

Mkurugenzi Mkuu wa Afrika Katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran pia amejadili masuala ya kieneo na kimataifa katika mkutanao wake na wakuu wa Kodivaa.

Katika kikao hicho Waziri wa Mambo ya Nje wa Ivory Coast amekubali mwaliko wa kuitembelea Iran na pia amesisitiza udharura wa kufanyika kikao cha pili cha Tume ya Pamoja ya Nchi Mbili.

Amesema Iran na Ivory Coast zinaweza kuimarisha uhusiano katika nyanja mbali mbali.