Iran yatuma wajumbe wa Quráni katika nchi mbalimbali duniani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i29602-iran_yatuma_wajumbe_wa_quráni_katika_nchi_mbalimbali_duniani
Kama ilivyo ada yake ya kila mwezi mtukufu wa Ramadhani, mwaka huu pia, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itatuma ujumbe mbalimbali wa Quráni katika nchi tofauti za dunia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 25, 2017 23:29 UTC
  • Iran yatuma wajumbe wa Quráni katika nchi mbalimbali duniani

Kama ilivyo ada yake ya kila mwezi mtukufu wa Ramadhani, mwaka huu pia, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itatuma ujumbe mbalimbali wa Quráni katika nchi tofauti za dunia.

Shirika la habari la IRNA limemnukuu Mehdi Ghare Sheikh Loo, mkuu wa taasisi ya Quráni Tukufu ya Iran akisema hayo jana mjini Bushehr na kuongeza kuwa, wajumbe hao tofauti wanajumuisha watu waliohifadhi Quráni Tukufu na maqarii wa kimataifa na watatumwa katika nchi mbalimbali za Ulaya, Afrika na Asia.

Qarii wa kimataifa wa Iran, Abbas Hashemi

 

Sheikh Loo ameongeza kuwa, Abbas Hashemi, qarii wa kimataifa kutoka mkoani Bushehr, (kusini magharibi mwa Iran) ametumwa katika mji mkuu wa Russia, Moscow, na atakuwa na ratiba mbalimbali za kusoma Quráni Tukufu kwa muda wa siku 20.

Amesema, lengo la kutumwa wajumbe tofati wa aina hiyo ni kupanua wigo wa harakati za Kitabu cha Mwenyezi Mungu, Quráni Tukufu na jambo hilo linalofanyika kila mwaka limekuwa na nafasi muhimu sana katika kueneza mafundisho ya Quráni Tukufu kwenye kona mbalimbali za dunia.