Hilali Nyekundu ya Iran kutuma misaada kwa Waislamu wa Rohingya
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i34041-hilali_nyekundu_ya_iran_kutuma_misaada_kwa_waislamu_wa_rohingya
Shirika la Hilali Nyekundu la Jamhuri ya Kiislamau ya Iran limesema limeandaa misaada ya kibinadamu kwa ajili ya Waislamu wa kabila la Rohingya nchini Myanmar.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Sep 07, 2017 14:33 UTC
  • Hilali Nyekundu ya Iran kutuma misaada kwa Waislamu wa Rohingya

Shirika la Hilali Nyekundu la Jamhuri ya Kiislamau ya Iran limesema limeandaa misaada ya kibinadamu kwa ajili ya Waislamu wa kabila la Rohingya nchini Myanmar.

Mkuu wa shirika hilo, Morteza Salimi amesema baada ya kupewa agizo na Rais Hassan Rouhani wa Iran, wameandaa mashehena ya tani 40 ya misaada ya kibindamu yenye bidhaa kama chakula, madawa na suhula za usafi kwa ajili ya Waislamu wanaonyongeshwa wa Myanmar.

Afisa huyo wa Shirika la Hilali Nyekundu la Jamhuri ya Kiislamau ya Iran ameongeza kuwa, kwa sasa wanasubiri idhini ya serikali ya Myanmar ili waweza kusafirisha misaada hiyo ya kibinadamu.

Rais Hassan Rouhani wa Iran

Hapo jana Rais wa Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kulaani mauaji ya Waislamu wa Myanmar na kuitaka serikali ya nchi hiyo izuie jinai zinazofanywa dhidi ya Waislamu hao alisema utumiaji silaha ya mauaji ya kimbari hauwezi kukubalika katika dunia ya leo na kuwa, Waislamu wa Myanmar na Waislamu wengine duniani; na Iran, ikiwa ni nchi ya Waislamu na ya kimapinduzi inajihisi ina jukumu kuhusiana na wanaodhulumiwa duniani hata kama watakuwa si Waislamu.

Taarifa zinasema zaidi ya Waislamu 3,000 wameuawa kwa umati tokea Agosti 25 wakati wa kuanza wimbi jipya la ukatili wa jeshi katika jimbo lenye Waislamu wengi la Rakhine nchini Myanmar, mbali na wengine zaidi ya laki moja na nusu kukimbilia Bangladesh.