Ayatullah Ahmad Jannati: Hatua yoyote iliyo dhidi ya Uislamu itashindwa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i38111-ayatullah_ahmad_jannati_hatua_yoyote_iliyo_dhidi_ya_uislamu_itashindwa
Ayatullah Ahmad Jannati, Katibu wa Baraza la Kulinda Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, hatua yoyote ile iliyo dhidi ya Uislamu na Waislamu itashindwa na kusambaratika.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 26, 2017 00:16 UTC
  • Ayatullah Ahmad Jannati: Hatua yoyote iliyo dhidi ya Uislamu itashindwa

Ayatullah Ahmad Jannati, Katibu wa Baraza la Kulinda Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, hatua yoyote ile iliyo dhidi ya Uislamu na Waislamu itashindwa na kusambaratika.

Ayatullah Jannati amesema hayo hapa mjini Tehran alipokutana na wahadhiri na wanachuo wenye vipawa wa Lebanon na kueleza kwamba, kundi la kigaidi la Daesh limeshindwa na kusambaratishwa na vikosi vya Kiislamu na kufukuzwa kutoka katika nchi za Iraq na Syria.

Akiwahutubu hadhirina, Katibu wa Baraza la Kulinda Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa: Muda si mrefu mtashuhudia kuanguka utawala bandia wa Israel na kkushindwa huku sio makhsusi kwa maghasibu tu bali Marekani na waungaji mkono wake nao watakumbwa na hili.

Rais Donald Trump wa Marekani

Ayatullah Ahmad Jannati ameashiria hatua ya Rais wa Marekani Donald Trump ya kuitangaza Beitul-Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala ghasibu wa Israel na kkueleza kuwa, hatua hiyo ya Trump ambayo imekabiliwa na malalamiko na upinzani wa Waislamu na hata wasiokuwa Waislamu ni kitendo kilicho mbali na akili na kisichokuwa cha kimantiki.

Aidha Ayatullah Jannati ametanabahisha kwamba, kushindwa na kusambaratika utawala haramu wa Israel na waungaji mkono wake si jambo lisilowezekana na kwamba, tawala hizo zitajiangamiza kwa mikono yao zenyewe.