Rouhani: Ulimwengu una imani kamili na Iran, Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu
(last modified Tue, 13 Feb 2018 16:48:13 GMT )
Feb 13, 2018 16:48 UTC
  • Rouhani: Ulimwengu una imani kamili na Iran, Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "Ulimwengu una imani kamili na Iran, Mapinduzi na Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu."

Rais Hassan Rouhani ameyasema hayo leo mjini Tehran katika kikao cha pamoja cha wakuu wa mikoa, mawaziri pamoja na wakuu wa taasisi za kiuchumi na kifedha nchini. Katika hotuba yake, Rais Rouhani amehoji hivi: 'Ni kwa nini ulimwengu ulisimama kidete mbele ya rais Donald Trump wa Marekani wakati alipotangaza kupinga JCPOA (mapatano ya nyuklia ya Iran)? Rais Rouhani amesema laiti kama mfumo na mustakabali wa Iran usingekuwa imara, zaidi ya nchi 190 duniani zisingesimama kidete kumpinga Trump na kwa hivyo kusimama kidete huko ni ishara ya kuwa dunia ina imani na mfumo wa Kiislamu, taifa na serikali ya Iran.

Ameendelea kusema kuwa itibari ya Iran inazidi kuimarika duniani na kuongeza kuwa hivi karibuni shirika la kimataifa linalotathmini hatari ya uwekezaji lilitangaza kupungua kiwango cha hatari hiyo kwa upande wa Iran kutoka kiwango cha asilimia saba hadi asilimia tano na hilo linaonyesha itibari ya Jamhuri ya Kiislamu inazidi kuongezeka. 

Rais  Rouhani katika kikao cha pamoja cha wakuu wa mikoa, mawaziri, wakuu wa taasisi za kiuchumi na kifedha, Tehran 13/02/2018

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia ameashiria kutokuwa na athari propaganda za adui dhidi ya Iran na kusema,  ustawi wa kiuchumu wa Iran baina ya Machi 2017 hadi Machi 2018 utakuwa wa juu zaidi ya wastani wa dunia.

Rais Rouhani pia amewashukuru wananachi wa Iran kwa kujitokeza kwa wingi katika maandamano ya Februari  11 ya maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Tags