Rais Rouhani: Tukijilegeza mbele ya mabeberu hatutofika popote
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i44942-rais_rouhani_tukijilegeza_mbele_ya_mabeberu_hatutofika_popote
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, heshima, utukufu, staha na hadhi ndiyo mambo muhimu zaidi kwa taifa kabla ya jambo lolote na kuongeza kuwa, hata kama tutakuwa na taifa tajiri lenye watu wengi lakini tukawa dhalili mbele ya dola fulani la kibeberu, basi hatutoweza kufika popote.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
May 24, 2018 23:50 UTC
  • Rais Rouhani: Tukijilegeza mbele ya mabeberu hatutofika popote

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, heshima, utukufu, staha na hadhi ndiyo mambo muhimu zaidi kwa taifa kabla ya jambo lolote na kuongeza kuwa, hata kama tutakuwa na taifa tajiri lenye watu wengi lakini tukawa dhalili mbele ya dola fulani la kibeberu, basi hatutoweza kufika popote.

Rais Rouhani amesema hayo usiku wa kuamkia leo katika kongamano la kuwaenzi watu wanaojitolea katika njia ya haki hususan mashahidi wa ukombozi wa mji wa Khoramshahr wa kusini magharibi mwa Iran ukombozi ambao unaadhimishwa tarehe 24 Mei kila mwaka. 

Rais Rouhani amegusia namna rais wa Mrekani alivyowatukana wananchi wa Saudi Arabia kwa kuwaita kuwa eti ni ng'ombe wa kukamuliwa maziwa tu na kutangaza kwa jeuri kuwa lazima ng'ombe hao wakamuliwe maziwa, na kuongeza kuwa: Utajiri na maisha mazuri ni kitu kizuri kwa taifa, lakini lililo muhimu zaidi ni heshima, hadhi na utukufu.

Picha iliyopigwa muda mchache baada ya kukombolewa Khorramshahr na kufurushwa wanajeshi vamizi wa Saddam tarehe 24 Mei 1982

 

Amesema kama si kujitolea wanamapambano wa Kiislamu kulinda mipaka na ardhi ya Iran pamoja na heshima, Uislamu na Mapinduzi ya Kiislamu, haijulikani leo hii tungelikuwa katika hali gani. Ameongeza kuwa, tumeona katika miaka ya hivi karibuni namna magaidi walivyozichezea na kuzitia hatarini roho, mali na heshima za wananchi wa Iraq na Syria.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa, leo hii taifa la Iran linahesabiwa kuwa ni taifa kubwa lenye heshima duniani kwani limetawakali kwa Mwenyezi Mungu na kushikamana na mafundisho ya Mtume Muhammad SAW na maimamu watoharifu na kusimama kidete kujihami mbele ya maadui.