Waislamu wakumbuka mauaji ya mjukuu wa Mtume (saw), Imam Ridhaa (as)
Mamilioni ya Waislamu wapenzi wa Watu wa Nyumba ya Mtume wetu Muhammad (saw) tangu usiku wa kuamkia leo tarehe 29 Safar wanaendelea kukusanyika katika misikiti, taasisi za kidini na kumbi za masuala ya kijamii wakikumbuka mauaji ya mjukuu wa Mtume wetu muhammad (saw), Imam Ali bin Mussa al Ridhaa (as).
Shughuli ya kukumbuka mauaji ya mjukuu huyo wa Mtume inaendelea kufanyika katika nchi mbalimbali hususan Iraq, Pakistan, Bahrain, Iran, Lebanon, Kuwait na mashariki mwa Saudi Arabia.
Nchini Iran mamilioni ya Waislamu jana usiku walikusanyika katika maeneo mbalimbali kukumbuka mauaji ya mtukufu huyo usiku wa kumkia tarehe 29 Safar.
Shughuli ya kukumbuka mauaji ya Imam Ridhaa (as) ilikuwa kubwa zaidi katika miji mitakatifu ya Qum na Mash'had ambako waumini walioneka kuvaa mavazi yenye rangi nyeusi kama ishara ya maombolezo.
Shughuli ya kukumbuka mauaji ya mjukuu huyo wa Mtume (saw) inaendelea leo kote nchini Iran na maeneo mengine ya dunia.
Imam Ali bin Musa al Ridhaa aliawa shahidi tarehe 29 Safar miaka 1236 ibaada ya kupewa sumu na mtawala Maamun wa ukoo wa Bani Abbas.