Mazungumzo ya Iran, Russia na Uturuki kuhusu katiba ya Syria
(last modified Tue, 18 Dec 2018 07:36:19 GMT )
Dec 18, 2018 07:36 UTC
  • Mazungumzo ya Iran, Russia na Uturuki kuhusu katiba ya Syria

Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran leo ameelekea Geneva, Uswisi kwa lengo la kushiriki katika kikao cha pande tatu kuhusu katiba ya Syria

Kikao hicho cha pande tatu kuhusu kamati ya katiba ya Syria kinahudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje ya Russia Sergei Lavrov na Waziri wa Mambo ya Nje ya Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu chini ya uenyekiti wa Staffan de Mistura, mjumbe maalimu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Syria.

Hapo jana Sadeq Hussien Jaber Ansari, msaidizi wa ngazi za juu wa Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran alikutana na kufanya mazungumzo na Rais Bashar al Assad wa Syria mjini Damascus na walijadili kuhusu matukio ya hivi karibuni yanayohusu kuanzishwa kamati ya kuandika katiba mpya ya Syria.

Rais Assad wa Syria

Wiki iliyopita, mjumbe maalumu wa Rais Vladimir Putin wa Russia katika masuala ya Syria  Alexander Lavrentiev alikuwa safarini mjini Tehran na ambapo alibadilishana mawaziri na maaafisa wa Iran kuhusu Syria.

Mgogoro wa Syria ulianza mwaka 2011 baada ya hujuma kubwa ya magaidi wanaopata himaya ya Saudia Arabia, Marekani na waitifaki wao kwa lengo la kubadilisha mlingano wa nguvu katika eneo  hili kwa maslahi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.