Rais Rouhani aomboleza kifo cha Ayatullah Shahroudi
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma salamu za rambirambi kufuata kuaga dunia Ayatullah Sayyid Mahmoud Hashemi Shahroudi, mwenyekiti wa Baraza la Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na mkuu wa zamani vya Vyombo vya Mahakama Iran.
Katika ujumbe wake, Rais Rouhani amesema amesikitishwa na kifo cha cha Ayatullah Shahroudi na kumtaja kuwa mwanazuoni aliyeandika vitabu vingi vyenye manufaa kwa lengo la kuinua utamaduni na ustaarabu wa Kiislamu na Iran.
Aidha amemtaja kuwa mwanazuoni aliyejitahidi kukurubisha vyuo vikuu vya kidini vya vyuo vikuu na kawaida na pia alijitahidi kustawisha sayansi za kijamii ambapo katika fremu hiyo aliasisi Chuo Kikuu cha Edalat.
Ayatullah Shahroudi, amefariki dunia jana Jumatatu, Disemba 24, 2018 akiwa na umri wa miaka 70 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Ayatullah Sayyid Mahmoud Hashemi Shahroudi alizaliwa tarehe 15 Agosti 1948 katika mji wa Najaf nchini Iraq na alikuwa miongoni mwa wanafunzi wakubwa wa shahid Ayatullah Sayyid Muhammad Baqir.