Marekani yaendeleza propaganda chafu dhidi ya Iran
(last modified Sat, 02 Mar 2019 08:06:10 GMT )
Mar 02, 2019 08:06 UTC
  • Marekani yaendeleza propaganda chafu dhidi ya Iran

Makamu wa Rais wa Marekani amekariri madai yasiyo na msingi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusisitiza kuwa, serikali ya Washington itaendeleza misimamo na hatua zake dhidi ya Iran.

 Kwa mara nyingine tena Mike Pence ameunga mkono uamuzi wa Rais Donald Trump wa Marekani wa kujiondoa katika makubaliano ya kimataifa ya nyuklia kati ya Iran na nchi za kundi la 5+1 zikiwemo nchi wanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kuyataja makubaliano hayo yaliyoidhinishwa na Umoja wa Mataifa kuwa ni "maafa". 

Ijumaa ya jana Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran Muhammad Javad Zarif alitetea tena makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kusema ni matunda ya miaka kumi ya "mpambano na mazungumzo". Zarif alimwambia Donald Trump kwamba, kamwe hawezi kupata makubaliano bora kuliko hayo.

Zarif (kulia) na Donald Trump

Itakumbukwa kuwa tarehe 8 Mei mwaka jana wa 2018 Rais Donald Trump alichukua hatua ya upande mmoja na kukika mapatano ya kimataifa ya nyuklia ya JCPOA na kutangaza tena vikwazo vinavyohusiana na faili la nyuklia dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu. Hatua hiyo ilikabiliwa na malalamiko na ukosoaji mkubwa katika upeo wa kimataifa zikiwemo nchi waitifaki wa Marekani barani Ulaya kama Uingereza na Ufaransa.   

Tags