Meja Jenerali Hussein Salami: Adui ataendelea kulegeza msimamo mbele ya Iran
Meja Jenerali Hussein Salami, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) amesema kuwa, ni lazima adui ataendelee kulegeza msimamo madhali matakwa halali ya taifa hili hayajatambuliwa rasmi.
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) amesema hayo huko katika mkoa wa Khuzestan kusini magharibi mwa Iran na kueleza wazi kuwa, maadui wanapaswa kuheshimu irada ya taifa la Iran na kwamba, hakuna mtu anayeweza kulitwisha taifa hili fikra na mitazamo yake.
Meja Jenerali Hussein Salami amesisitiza kuwa, Iran katu haitasalimu amri katika mazingira yoyote yale na kuongeza kwamba, mashinikizo na vikwazo si njia ya kukabiliana na Iran.
Amesema, hii leo mataifa ambayo yalikuwa yakijigamba kwa kusema hayataruhusu hata tone moja la mafuta ya Iran kuuzwa nje, sasa yamelegeza msimamo wao.
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) amewaonya maadui ajinabi juu ya kuilenga izza na heshima ya taifa la Iran na kusisitiza kwamba, endapo dola la Uingereza ambalo lina nafasi kubwa katika kuirejesha nyuma Iran litataka kuivimbishia misuli Tehran, basi vijana wa taifa hili wataitoa meli yake baina ya meli nne za Marekani na Uingereza na kuileta ufukweni; na ni wakati huo ambapo kile kinachoonekana kama haiba na ukubwa wa ustikbari unaposambaratika.