Rouhani: Iran ina uwezo wa kuunda vifaa vya vituo vya kuzalisha umeme
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i57214-rouhani_iran_ina_uwezo_wa_kuunda_vifaa_vya_vituo_vya_kuzalisha_umeme
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria mafanikio makubwa ya kisayansi nchini Iran na kusema: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hivi sasa ina uwezo mkubwa katika kuunda vifaa na mashine zinazotumika katika vituo vya kuzalisha umeme."
(last modified 2026-03-27T07:58:19+00:00 )
Nov 12, 2019 01:47 UTC
  • Rouhani: Iran ina uwezo wa kuunda vifaa vya vituo vya kuzalisha umeme

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria mafanikio makubwa ya kisayansi nchini Iran na kusema: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hivi sasa ina uwezo mkubwa katika kuunda vifaa na mashine zinazotumika katika vituo vya kuzalisha umeme."

Rais Rouhani ameyasema hayo Jumatatu katika sherehe za kuzinduliwa miradi ya madini, chuma na sekta za maji na umeme katika mkoa wa Kerman kusini mwa Iran.  Ameongeza kuwa,  kumeibuliwa harakati kubwa katika sekta ya uzalishaji umeme nchini Iran kwani hivi sasa si tu kuwa Iran inajijengea kikamilifu vituo vya kuzalisha umeme bali pia inazisaidia nchi za kieneo katika sekta hiyo.

Rais Rouhani ameashiria namna ambavyo Iran imeweza kupiga hatua kubwa za maendeleo katika kipindi cha miaka 40 iliyopita baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuongeza kuwa: "Leo Iran ina uwezo mkubwa katika sekta za viwanda vya chuma, ujenzi wa reli, mafuta na gesi, petrokemikali, uchimbaji na usafishaji mafuta."

 Bwawa la Karun-3 Katika Mto Karun Mkoani Khuzestan , Iran.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aidha ameashiria uwezo mkubwa wa Iran katika uundaji makombora ya kujihami na kusema: "Leo katika sekta ya ulinzi wa angani Iran imefika kiwango ambacho inaunda makombora ambayo yanatungua ndege isiyo na rubani (drone) ya Marekani."

Halikadhalika Rais Rouhani amesema, mafanikio ya Iran yametokana na kustahamili magumu, jitihada, imani, na kujitolea taifa la Iran na kuongeza kuwa: "Ili kuweza kupata mafanikio zaidi ya maendeleo, kasi ya ustawi na ujenzi wa miundo msingi ya Iran ya Kiislamu inapaswa kuongezeka."