Rouhani: Kumefikiwa mapatano mazuri sana huko Malaysia na Japan
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambaye alielekea Malaysia na Japan kufuatia mwaliko rasmi wa Mawaziri Waku wa nchi hizo jana alasiri alirejea Tehran.
Baada ya kuwasili Tehran, Rais Hassan Rouhani amesema kuwa ziara yake huko Malaysia na Japan ina umuhimu mkubwa katika kipindi hiki na kwamba wamefikia makubaliano mazuri sana katika ziara zake huko Malaysia na Japan.
Rais Rouhani ameashiria kikao cha viongozi wa nchi za Malaysia, Iran, Uturuki na Qatar pambizoni mwa Mkutano wa Kuala Lumpur na kueleza kuwa: Maamuzi mazuri sana yamechukuliwa katika mkutano huo kwa ajili ya kushirikiana nchi hizo nne na bila shaka nchi nyingie pia zilialikwa kujadili suala la ustawi khususan katika sekta ya ushirikiano wa teknolojia za kisasa na katika sekta za viwanda.

Rais wa Iran ameongeza kuwa kikao cha pamoja cha ushirikiano kati ya Iran na Malaysia kinatazamiwa kufanyika siku chache zijazo na kwamba Mahatir Muhammad Waziri Mkuu wa Malaysia ana hamu ya kuitembelea Iran hivi karibuni.
Wakati huo huo Rais Rouhani ameashiria tangazo la kuwa tayari Abe Shinzo Waziri Mkuu wa Japan kuwekeza katika eneo la Chabahar na kueleza kuwa suala la njia ya usafiri ya kusini hadi kaskazini ambayo inaanzia Chabahar, kusini mashariki mwa Iran hadi bahari ya Caspian (Kaspi); na kuanzia hapo kuendelea hadi Turkmenistan, Incheboron na Astara lina umuhimu mkubwa kwa Wajapani.