Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu apongeza utendaji kazi wa IRGC
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i60528-kiongozi_muadhamu_wa_mapinduzi_ya_kiislamu_apongeza_utendaji_kazi_wa_irgc
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma ujumbe maalumu na kupongeza utendaji kazi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC.
(last modified 2026-07-03T11:45:53+00:00 )
Apr 22, 2020 02:40 UTC
  • Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu apongeza utendaji kazi wa IRGC

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma ujumbe maalumu na kupongeza utendaji kazi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC.

Kwa mujibu wa tovuti ya Sepah News, Brigedia Jenerali Mohammad Shirazi Mkuu wa Ofisi ya Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Iran amempigia simu Meja Jenerali Hussein Salami Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kumtumia ujumbe wa Ayatullah Sayyed Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Iran, kwa munasaba wa siku ya kuasisisiwa IRGC.

Katika mazungumzo hayo ya simu,  Brigedia Jenerali Shirazi amesema, Ayatullah Khamenei ametoa shukrani zake za dhati na kupongeza utendaji kazi na jitihada nzuri za IRGC. 

Meja Jenerali Hussein Salami Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu

Tarehe 21 Aprili miaka 41 iliyopita Imam Khomeini (M.A) mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alitoa amri ya kuundwa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC). Kwa mujibu wa amri hiyo, jukumu kuu la jeshi hilo ni kulinda Mapinduzi ya Kiislamu dhidi ya maadui wa ndani na nje