Mousavi: Siku ya Hilali/Msalaba Mwekundu inakumbusha kuhusu kukabiliana na vitisho duniani
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma salamu za pongezi kwa munasaba wa Siku ya Hilali Nyekundu na Msalaba Mwekundu Duniani na kusema: "Siku ya Hilali Nyekundu na Msalaba Mwekundu Duniani inakumbusha kuhusu vigezo vya msingi katika kukabiliana na vitisho duniani.
Sayyid Abbas Mousavi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametuma ujumbe kupitia ukurasa wake wa Twitter Ijumaa na kuandika kuwa: "Mashikamano, ushirikiano na maamuzi ya pande kadhaa ni mambo ambayo hayawezi kuangamizwa na matukio kama vile janga la COVID-19, sera za kuchukua maamuzi ya upande mmoja au msururu wa vikwazo."

Tarehe nane ya kila mwezi Mei inatambuliwa kuwa siku ya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu. Msalaba Mwekundu ni shirika la kimataifa ambalo liliundwa kwa ajili ya kutuliza machungu ya wanadamu na kulinda maendeleo ya sekta ya afya ya kijamii kwa mujibu wa mkataba wa Geneva, Uswisi hapo mwaka 1864 Miladia. Katika nchi za Kiislamu shirika hilo linaitwa kwa jina la Hilali Nyekundu.