Mousavi: Iran haitasalimu amri mbele ya vikwazo vya kukaririwa vya Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i61516-mousavi_iran_haitasalimu_amri_mbele_ya_vikwazo_vya_kukaririwa_vya_marekani
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa viongozi wa Marekani wanajisumbua bure kwa vikwazo hivyo vipya na kwamba Iran katu haitasalimu amri mbele ya vikwazo na mashinikizo ya aina hii. Sayyid Abbas Mousavi ameyasema hayo kufuatia hatua ya Marekani ya kuyawekea vikwazo vipya makampuni ya meli na meli za kubeba mafuta za Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 10, 2020 03:50 UTC
  • Mousavi: Iran haitasalimu amri mbele ya vikwazo vya kukaririwa vya Marekani

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa viongozi wa Marekani wanajisumbua bure kwa vikwazo hivyo vipya na kwamba Iran katu haitasalimu amri mbele ya vikwazo na mashinikizo ya aina hii. Sayyid Abbas Mousavi ameyasema hayo kufuatia hatua ya Marekani ya kuyawekea vikwazo vipya makampuni ya meli na meli za kubeba mafuta za Iran.

Ofisi Kuu ya Fedha za Kigeni ambayo ni moja ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha ya Marekani hivi karibuni imeziwekea vikwazo kwa mara nyingine tena meli za mizigo na za mafuta za Iran ambazo tayari zilikuwa zipo katika orodha ya meli zilizo chini ya vikwazo vya wizara hiyo. 

Meli ya mafuta ya Iran 

Sayyid Abbas Mousavi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran leo amesema Marekani kwa wakati mmoja huliwekea vikwazo taifa zima la Iran na kisha katika kalibu ya vikwazo hivyo hivyo kuwawekea vikwazo raia na viongozi wa Iran mmoja mmoja. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje amesisitiza kuwa vikwazo vya upande mmoja na vilivyo kinyume cha sheria vya Marekani kabla ya kuidhuru Iran, vinawadhuru waitifaki wake yenyewe (Marekani) pamoja na biashara ya kimataifa. Ameongeza kuwa jamii ya kimataifa inapasa ifikirie na kuzuia vikwazo hivyo vya upande mmoja  vya Marekani dhidi ya nchi nyingine. 

Mousavi amesisitiza kuwa askari wa ulinzi wa mipakani wa Iran hawatasita wala kuzembea katika kulinda usalama wa taifa na kukumbusha kuwa: Baadhi ya raia wa nchi jirani na hata wasio jirani wanafanya kila wanaloweza kuingia nchini kinyume cha sheria; na polisi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitasita katika kulinda usalama wa taifa.