Velayati: Wamagharibi wanapanga kuzigawa vipande vipande Iraq, Syria
Afisa mwandamizi wa Iran amelaani vikali njama za nchi za Magharibi na waitifaki wao kieneo za kutaka kuzigawa vipande vipande Iraq na Syria.
Ali Akbar Velayati, Mshauri wa Kiongozi Muadhamu katika masuala ya kimataifa ameyasema hayo Jumapili mjini Tehran alipokutana na kufanya mazungumzo na Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Yan Kubish.
Velayati amesema njama hizo za kuzisamabratisha Iraq na Syrai hazitafaulu kutokana na kuwepo macho mrengo wa mapambano katika eneo.
Velayati aidha ametoa wito wa kupewa uzito suala la kupambana na ugaidi duniani.
Velayati, ambaye pia ni Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kiistratijia cha Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ametabiri kuwa uungaji mkono wa nchi za Maghribi ni suala ambalo hatimaye litamalizika kwa hasara ya nchi hizo.
Siku ya Jumamosi pia, Velayati alisema kuwa ndoto za maadui za kutaka kuzigawa na kuzidhibiti nchi za Kiislamu katika Mashariki ya Kati hazitafanikiwa.
Aliyasema hayo katika mazungumzo yake hapa mjini Tehran na Ramadhan Abdullah Shallah, kiongozi wa Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina na kubainisha kwamba, Iran itaendelea kuunga mkono taifa madhulumu la Palestina na mataifa yanayotendewa dhulma Mashariki mwa Asia.