Kamalvandi: Maswali ya IAEA yanapaswa kuzingatia vigezo na kuwa na ushahidi
(last modified Mon, 24 Aug 2020 03:14:29 GMT )
Aug 24, 2020 03:14 UTC
  • Behrouz Kamalvandi
    Behrouz Kamalvandi

Msemaji wa Shirika la Atomiki la Iran amesema kuwa, Tehran haiwazuii wakaguzi wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) kutembelea vituo vyake vya nishati ya nyuklia lakini maswali yanayoulizwa na wakala huo yanapaswa kuzingatia vigezo na kuwa na ushahidi wa kutosha.

Behrouz Kamalvandi ameashiria madai kwamba Tehran haishirikiani na wakala wa IAEA na kusema kuwa: Maswali yanayoambatana na ripoti za kijasusi na mfano wake hayakubaliki na sharti muhimu katika uwanja huo ni kwamba maswali yaulizwe mara moja na si kukaririwa mara kwa mara.

Hivi karibuni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki, Rafael Grossi‎ alitoa ripoti akidai kuwa, Iran imewazuia wakaguzi wa wakala huo kukagua maeneo mawili ya nishati ya nyuklia. Madai yaliyotolewa kuhusiana na maeneo hayo yametegemea ripoti za kijasusi za utawala haramu wa Israel. 

Rafael Grossi‎ anatazamiwa kuwasili nchini Iran leo Jumatatu. 

Msemaji wa Shirika la Atomiki la Iran amesema inatarajiwa kwamba safari hiyo itaondoa dukuduku na wasiwasi wa pande mbili.  

Tags