Waliopona COVID-19 Iran wapindukia 420K
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i64051-waliopona_covid_19_iran_wapindukia_420k
Msemaji wa Wizara ya Afya ya Iran Sima Sadat Lari ametangaza kuwa hadi sasa watu 522,387 wameambukizwa corona nchini Iran na miongoni mwao 420, 910 wamepona.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Oct 16, 2020 08:43 UTC
  • Msemaji wa Wizara ya Afya ya Iran Sima Sadat Lari
    Msemaji wa Wizara ya Afya ya Iran Sima Sadat Lari

Msemaji wa Wizara ya Afya ya Iran Sima Sadat Lari ametangaza kuwa hadi sasa watu 522,387 wameambukizwa corona nchini Iran na miongoni mwao 420, 910 wamepona.

Kwa mujibu wa taarifa ya siku ya Ijumaa, idadi ya walioambukizwa corona katika masaa 24 yaliyopita ni 4,552 na miongoni mwao 2,016 wamelazwa hospitalini.

Aidha amesema katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita watu 265 wamepoteza maisha nchini Iran kutokana na corona na hivyo idadi jumla ya waliopoteza maisha nchini ni 29,870. 

Katika upande mwingine hadi kufikia leo mchana, idadi ya watu waliokumbwa na kirusi cha corona duniani kote imepindukia milioni 39,251,396. Miongoni mwa hao, watu zaidi ya 1,104,159 wameshaaga dunia na wengine karibu milioni 29,421,849 wamepata nafuu na kuruhusiwa kutoka hospitalini.

Marekani imeendelea kuwa nchi iliyoathiriwa zaidi na kirusi cha corona duniani baada ya karibu watu milioni 9 kuambukizwa kirusi hicho, ikifuatiwa na India, Brazil, Russia na Uhispania