"Shahidi Qassem Suleimani aliugeuza muqawama kuwa harakati ya ulimwengu mzima"
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i66442-shahidi_qassem_suleimani_aliugeuza_muqawama_kuwa_harakati_ya_ulimwengu_mzima
Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema, shahidi kamanda Qassem Suleimani aliugeuza muqawama kuwa harakati ya ulimwengu mzima.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 04, 2021 00:57 UTC

Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema, shahidi kamanda Qassem Suleimani aliugeuza muqawama kuwa harakati ya ulimwengu mzima.

Sheikh Naim Qassem amefafanua kuwa, shahidi Qassem Suleimani, kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, aliuchukulia muqawama kuwa ni majimui iliyokamilika kinadharia, kwa maana ya vuguvugu la harakati, imani na uelewa wa kiutamaduni na kisiasa ambao una taathira ya moja kwa moja kwa utendaji wa wanajihadi na mafanikio kwa umma wa Kiislamu.

Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameongeza kuwa, shahidi Suleimani aliubadilisha muqawama uliokuwa harakati ya kiutaifa ndani ya Iran na kuugeuza kuwa harakati ya ulimwengu mzima; ukawa ni vuguvugu la dunia nzima pasi na kukiuka utambulisho wa nchi zenyewe. 

Sheikh Naim Qassem

Sheikh Naim Qassem amesisitiza kuwa, kwa mtazamo wa Haj Qassem Suleimani Marekani ndilo tatizo kuu, kwa sababu inautumia utawala wa Kizayuni ili kuvuruga uthabiti wa eneo na muelekeo wa dira ya mhimili wa muqawama, yaani kadhia ya Palestina.

Luteni Jenerali Qassem Suleimani, kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, ambaye mnamo Januari 3, 2020 alielekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo, aliuawa shahidi katika shambulio la kigaidi la anga lililofanywa na jeshi vamizi na la kigaidi la Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad.../