Jun 09, 2021 12:15 UTC
  • Rais Rouhani: Uwezo wa Iran wa kuzalisha bidhaa za petrokemikali umeongezeka maradufu

Rais Hassan Rouhani amesema kuwa uwezo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa kuzalisha bidhaa za petrokemikali umeongezeka maradufu hivi sasa.

Rais Rouhani amesema hayo leo katika kikao cha Baraza la Mawaziri na kuongeza kuwa, uwezo wa kuuza nje bidhaa za petrokemikali nchini Iran leo hii ni karibu dola bilioni 22 kwa mwaka. 

Amesema, leo hii Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepandisha kiwango cha uzalishaji wa petroli kutoka lita milioni 56 na kufikia lita milioni 107 kwa siku. Uzalishaji wa dizeli pia pia umeongezeka nchini Iran kutoka lita milioni 97 hadi milioni 137 kwa siku.

Licha ya ugaidi mkubwa wa kiuchumi inaofanyiwa na Marekani, lakini Iran iko imara

 

Rais Rouhani pia amesema, wafanyakazi serikalini wana wajibu wa kuendeleza kwa nguvu zote kazi zilizofanywa na serikali zilizopita, kuanzia wiki za kwanza kabisa za kuingia madarakani rais mpya na kwamba kazi yoyote ambayo itasaidia kutatua matatizo yaliyopo, ni lazima ifanyike.

Rais Rouhani aidha amesema, ni matumaini yangu kwamba wananchi wa Iran watajitokeza kwa wingi na kwa hamasa kubwa katika uchaguzi na watachagua kiongozi anayefaa zaidi kuwa Rais wa baadaye wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Rais atakayekuja pia ataweza kuunda serikali madhuguti na kuweza kuwanufaisha wananchi wa wa matabaka na rika zote.

Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Rais Hassan Rouhani hawezi kushiriki kwenye uchaguzi huu wa 13 wa rais humu nchini kwani ameshahudumu vipindi viwili mfululizo.

Tags