Jun 17, 2021 16:08 UTC
  • Rouhani: Tujitokeze kwa wingi kupiga kura ili tusiruhusu kutimia ndoto za adui

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa mara nyingine ametoa mwito kwa wananchi wa Iran kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi akisisitiza kuwa, kwa kushiriki vilivyo katika uchaguzi, taifa la Iran halitoruhusu kuaguka ndoto za adui.

Rais Hassan Rouhani ameeleza hayo leo Alkhamisi na kuongeza kuwa; maadui wanataka kuona uchaguzi wa Iran unakuwa baridi na akasema kuhudhuria kwa wingi wananchi katika masanduku ya kupigia kura kutakwamisha kufikiwa ndoto za adui. Rais Rouhani amesema; kesho Ijumaa tarehe 28 Khordad ambayo ni sawa na tarehe 18 Juni ni siku muhimu sana kwa taifa la Iran.  

Rais wa Iran amebainisha kuwa; Kura za wananchi na kushiriki kwao kwa wingi katika uchaguzi kuna taathira kubwa ya kumuwezesha  Rais atakayechaguliwa, kutatua matatizo ya ndani na pia masuala ya kimataifa na kutampa nguvu na uwezo mkubwa.  

Wananchi wa Iran na uchaguzi wa Rais  Juni 18, 2021 

Ameongeza kuwa, ni muhimu sana kwa wananchi wa matabaka yote ya chini amma ya juu, kushiriki katika uchaguzi; na wote kesho wanapaswa kutekeleza wajibu wao kwa kuelekea kwa wingi kwenye masanduku ya kupigia kura.  

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza pia kuwa, anataraji kuwa nchi hii itaendesha uchaguzi kwa mafanikio na tarehe 28 Khordad yaani Juni 18 isajiliwe kwa uzuri kama siku ya ukurasa mwingine katika kurasa za historia ya Mapinduzi ya Kiislamu. Duru ya 13 ya uchaguzi wa Rais wa Iran itafanyika kesho Ijumaa tarehe 18 mwezi Juni. 

Tags