Suleimani: Iran imeisaidia Syria kuirejesha nyuma Daesh
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i7717-suleimani_iran_imeisaidia_syria_kuirejesha_nyuma_daesh
Meja Jenerali Qassim Suleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds kinachofungamana na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC amesema magaidi wa Daesh wangekuwa tayari wameshaiteka Syria nzima kama usingelikuwa ni msaada wa Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 24, 2016 02:34 UTC
  • Suleimani: Iran imeisaidia Syria kuirejesha nyuma Daesh

Meja Jenerali Qassim Suleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds kinachofungamana na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC amesema magaidi wa Daesh wangekuwa tayari wameshaiteka Syria nzima kama usingelikuwa ni msaada wa Iran.

Suleimani amenukuliwa na shirika rasmi la habari la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRNA akisema katika mji mtakatifu wa Qum kwamba kama usingelikuwa ni msaada wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, hivi sasa ardhi yote ya Syria ingekuwa inadhibitiwa na magaidi wa kitakfiri wa Daesh. Suileimani pia amewashukuru washauri wa kijeshi wa Iran kwa kutoa roho zao kwa ajili ya kupambana na magaidi wa Daesh nchini Syria. Mapema mwezi huu jeshi la IRGC lilitangaza kwamba washauri wake wa kijeshi wapatao 13 wameuawa na wengine 21 kujeruhiwa katika mashambulio ya magaidi wa Daesh katika mji wa Khan Tuman ulioko kusini magharibi mwa mkoa wa Allepo. Jenerali Qassim Suleimani amesema washindi wa mapambano dhidi ya Daesh ni Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Amesema licha ya juhudi kubwa inazofanya, lakini Marekani haijaweza kufanikiwa katika kupunguza ushawishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika eneo hili nyeti la Mashariki ya Kati. Syria imekuwa ikikabiliwa na hujuma ya magaidi hao tokea mwaka 2011 ambapo serikali ya Damascus inazilaumu nchi za Saudi Arabia, Uturuki na Qatar kwa kushirikiana kwa karibu na Marekani katika kuvuruga uthabiti na usalama wa nchi hiyo kupitia magaidi wa Daesh wanaofanya uharibifu na mauaji ya kutisha katika ardhi ya nchi hiyo.