Meja Salami: Marekani imedhoofika
(last modified Wed, 24 Nov 2021 03:03:50 GMT )
Nov 24, 2021 03:03 UTC
  • Meja Salami: Marekani imedhoofika

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema: "Nguvu za Marekani zimedhoofika."

Meja Jenerali Salami, Kamanda Mkuu wa IRGC ameyasema hayo katika sherehe za kumbukumbu  ya kuasisiswa jeshi la kujitolea (Basiji) la wanafunzi na kuongeza kuwa, katika siku za mwanzo za uhai wa Mapinduzi ya Kiislamu, Marekani ilianzisha mkakati wa kuyaangusha mapinduzi hayo lakini ikawabinikia kuwa Iran ni kituo cha moyo wa dunia. Ameongeza kuwa, Wamarekani walifahamu kuwa nguvu za Iran hatimaye zitaidhoofisha Marekani. Aidha amesema hivi sasa Marekani inachukua maamuzi kwa kuizingatia Iran.

Kamanda Mkuu wa IRGC  amesema Jamhuri ya Kiislamu imapata mafanikio makubwa huku ikiwa na uhuru wa kisiasa na uhuru wa kujiamulia masuala ya kistratijia jambo ambalo limeipa fursa ya kujiainishia mustakabali wake. Aidha amesema uhuru wa kisiasa umepelekea Iran kupata uhuru katika nyuga za kiutamaduni, kiuchumi, kisayansi, kiusalama na kiulinzi.

Rais Biden wa Marekani

Meja Jenerali Salami amesema Mapinduzi ya Kiislamu yalipelekea uingiliaji wa kijeshi wa Marekani katika eneo usibadilika na kuwa nguvu za kisiasa. Kamanda wa IRGC amebainisha nukta hiyo kwa kusema Marekani imetumia zaidi ya dola trilioni 8 katika chokochoko zake za kijeshi katika eneo la Asia Magharibi lakini haikuweza kufikia malengo yake ya kijeshi katika eneo hilo.