Usitishaji vita waanza kutekelezwa huko Lebanon
Makubaliano ya kusitisha vita nchini Lebanon yamenza kutelezwa mapema leo saa kumi alfajiri kwa saa za Beirut.
Hatua hiyo inamaliza zaidi ya mwaka mmoja wa makabiliano ya kijeshi ya kuvuka mpaka na karibu miezi miwili ya vita vya wazi kati ya utawala wa kigaidi wa Israel na harakati ya Hizbullah ya Lebanon.
Baraza la mawaziri la Israel liliidhinisha usitishaji huo wa mapigano kufuatia miezi miwili ya mashambulizi makali dhidi ya Lebanon.
Kwa upande wa Lebanon, Bunge la nchi hiyo linatarajiwa kukutana leo Jumatano kujadili makubaliano hayo.
Licha ya tangazo la kuanza usitishaji vita huko Lebanon, uhasama ulipamba moto jana huku Israel ikizidisha mashambulizi yake ya anga katika mji mkuu, Beirut, na maeneo mengine ya Lebanon.
Hapo awali Hizbullah ilisema kuwa kukomeshwa kabisa uchokozi wa Israel dhidi ya Lebanon na kulindwa mamlaka ya nchi hiyo ndio masharti yake ya kukubali makubaliano yoyote ya kusitisha mapigano.
Makubaliano ya kusitisha mapigano yanalitaka jeshi la Israel kuondoka kusini mwa Lebanon, na jeshi la Lebanon kupelekwa katika eneo hilo.
Kiongozi wa upinzani katikak uutawala wa Kizayuni wa Israel, Yair Lapid amesema baraza la mawaziri la Benjamin Netanyahu "limeburutwa katika makubaliano na Hizbullah, na kwa sasa, miji ya kaskazini inaharibiwa, maisha ya wakazi wa maeneo hayo yameporomoka, na jeshi limechoka."