Raisi: Sheria ni mhimili wa kutekelezwa uadilifu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i77516-raisi_sheria_ni_mhimili_wa_kutekelezwa_uadilifu
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza katika kikao cha pamoja cha Serikali na Bunge kuwa sheria ndio mhimili wa kutekelezwa uadilifu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 01, 2021 04:54 UTC

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza katika kikao cha pamoja cha Serikali na Bunge kuwa sheria ndio mhimili wa kutekelezwa uadilifu.

Akizungumza leo Jumatano katika kikao cha pamoja cha Serikali na Bunge kwa mnasaba wa Siku ya Majlisi (Bunge), Rais Ebrahim Raisi amesema sheria ni mhimili wa uadilifu na kuwa kadiri sheria inavyotekelezwa kwa ukamilifu wake ndio uadilifu nao huwa umetekelezwa.

Huku akiashiria nafasi na jukumu kuu la bunge kuwa ni kubuni sheria, amesema kubuniwa kisheria ambayo inapaswa kufuatwa na wananchi ni jukumu la bunge, ambalo ni zito na muhimu mno.

Rais Raisi ameendelea kusema leo bunge ni dhihirisho halisi la irada na maoni ya wananchi na kuwa utungaji sheria ni sehemu ya majukumu ya bunge ambayo yanapaswa kutiiwa na kutekelezwa na wote.

Bunge la Iran

 

Rais Ebrahim Rais ameashiria kumbukumbu ya kuuawa Shahid Mudarres na maadhimisho ya Siku ya Bunge na kusema mfungamano uliopo kati ya umaanawi na siasa nchini ni sehemu muhimu zaidi ya maisha ya shakhsia huyo katika historia ya Iran.

Amesema dini inaweza kuongoza maisha ya mwanadamu na kukidhi mahitahi yake yote. Akizungumza katika kikao hicho Muhammad Bagher Qalibaf, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge) amesema anatumai serikali ya Raisi itafanikiwa katika juhudi zake za kuwaondolea wananchi wa Iran vikwazo vya kidhalimu vinavyotekelezwa na madola makubwa ya dunia.