Tarehe 12 Bahman, kumbukumbu ya kurejea Iran Imam Khomeini; kuanza Alfajiri Kumi
Jumanne ya jana tarehe 12 Bahman kwa mujibu wa kalenda ya Hijria Shamsia iliyosadifiana na tarehe Mosi Februaria 1979 ni siku ya kihistoria ambapo Imam Ruhullah Khomeini muasisi wa Jamhhuri ya Kiisloamu ya Iran alirejea hapa nchini baada ya kuwa uhamishoni kwa miaka 14.
Kurejea huku kwa Imam Khomeini ulikuwa ni utangulizi wa harakati isiyo na mithili ya wananchi na kufikia ushindi Mapinduzi ya Kiislamu, mapinduzi ambayo hayana mfano katika karne za hivi karibuni.
Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yanahhesabiwa kuwa mapinduzi muhimu na makubwa zaidi katika nusu ya pili ya karne ya 20 Miladia. Kuupata ushindi Mapinduzi ya Kiislamu kwa hakika ilikuwa ni kufikiwa irada na azma taifa kubwa kwa ajili yya kuujipatia mamlaka yya kujitawala, izza, hheshima na kuuondoka katika udhibiti na satwa ya madola ya kibeberu. Katika kipindi ambacho ulimwengu ulikuwa umegawanyyika kkatika kakmbi mbili kuu za magharibi na Mashariki, mapinduzi ya wananchi wa Iran yalikuwa yakipiga nara yay "Siyo Mashariki Wala Magharibi". Mapinduzi hayo ya Kiislamu yalipata ushindi tarehe 12 Februaria 1979 (22 Bahman 1357 Hijria Shamsia).
Kuanzia tarehe Mosi Februari hadi 12 ya mwezi huo mwaka 1979 siku mapinduzi hayo yalipopata ushindi yaani katika kipindi cha siku kumi kulitokea matukio nchini Iran ambayo yalipelekea kusambaratishwa mfumo wa fisadi wa utawala wa kifalme wa Shah. Siku hizi kumi zinazojulikana katika historia ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kwa jina la Alfajiri Kumi zilivuruga mahesabu yyote ya utawala wa Shah pamoja na waungaji mkono wake ikiwemo Marekani. Miongoni mipango michafu iliyogonga mwamba ni kushindwa njama za kuzuia kurejea nchini Imam Khomeini.
Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu anasema kuhusiana na siku hii kwamba: Tarehe 12 Bahman (Mosi Februari) kwa maana moja ni sikkuu ya kuanza nguvu ya Uislamu. Licha ya kuqwa katika tarehe hii kidhahiri mfumo wa kitaghuti ulikuwa madarakani, lakini uukweli wa mambo ni kuwa haukkuweko. Kimsingi ni kuwa, kurejea Imam Kkhomeini hapa nchini kulikwenda sambamba na kusambaratika mfumo huu fisadi. Wahusika walikuwa wakifanya juhudi zisizo na maana, ili waweze kuukoa mfumo huu ili ubakie tena kkwa siku kadhhaa, lakini hilo halikuwa likiwezekana na halikuwezekana.
Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yaliyopata ushindi kwa uongozi wa Imam Khomeini, hayawezi kulinganishwa na mapinduzi yoyote yale yaliyotokea katika mataifa mengine ya dunia katika pande zake mbalimbali za kisiasa, kiuchumi, kijamiii na kiutamaduni. Ukweli wa mambo ni kuwa, ukiacha Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran hakuna mapinduzi mengine yoyote yale duniani ambayo yana sifa na vigezo vya mapinduzi ya kweli ambayo ndani yake kuna itikadi zote, thamani za jamii ile na kuweko ushiriki wa matabaka yote ya jamii.
Imam Khomeini (RA) anasema kuhusiana na kulinganishwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na mapinduzi mengine ya dunia kwamba: Someni na mfanye utafiti kuhhusiana na mapinduzi ya Ufaransa na mapinduzi yale Sovieti. Watu waone kabla ya mapinduzi hayyo kulikuwa na nini na baada yya mapinduzi kuna nini. Je wananchi wamepata kituu kupitia mapinduzi hayo?
Imam Khomeini ambaye alikuwa na utambuzi kamili kuhusiana na hali ya kisiasa, kiutamaduni na jamii ya Iran katika miaka ya kupamba moto harakati za mapinduzi na kabla ya hapo, anatambua sababu kuu na siri ya mafanikio ya mapinduzi hayo mabadiliko ya kiroho na kiimani ya wananchi. Katika mazingira kama haya; wananchi wakabadilika kupitia hotuba na maneno ya Imam Khomeini sambamba na mapenzi ya Mwenyezi Mungu, wananchi hao wakawa hawana woga kwa utawala dhalimu wa Shah na ndio maana wakasimama kidete dhidi ya utawala huo..