Ulyanov: Ziara ya Rafael Grossi nchini Iran imefanikiwa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i81096-ulyanov_ziara_ya_rafael_grossi_nchini_iran_imefanikiwa
Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika taasisi za kimataifa zenye makao yake mjini Vienna, Austria amesema kuwa safari ya Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA) nchini Iran imefanikiwa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 07, 2022 00:47 UTC
  • Ulyanov: Ziara ya Rafael Grossi nchini Iran imefanikiwa

Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika taasisi za kimataifa zenye makao yake mjini Vienna, Austria amesema kuwa safari ya Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA) nchini Iran imefanikiwa.

Mkurugenzi Mkuu wa IAEA, Rafael Grossi juzi asubuhi aliwasili Tehran kwa lengo la kuonana na kuzungumza na viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu suala kuendeleza ushirikiano wa kiufundi baina ya pande mbili. Hii ni safari ya tatu ya Mkurugenzi Mkuu wa wakala wa IAEA hapa Tehran katika uongozi wa serikali ya 13 ya Iran. 

Rafael Grossi baada ya kuwasili Tehran na kulakiwa na Behrouz Kamalvandi 

Ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki mjini Tehran imefanyika wakati duru ya 8 ya mazungumzo kati ya Iran na kundi la 4+1 kwa ajili ya kuindolea Iran vikwazo dhidi yake ilivyowekewa na Marekani ikiendelea huko Vienna, Austria. 

Shirika la habari la Fars limeripoti kuwa, Mikhail Ulyanov Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika Taasisi za Kimataifa huko Vienna ameashiria ziara ya Grossi mjini Tehran na kueleza kuwa: Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki na Iran zimekubaliana juu ya hatua madhubuti za kutatua masuala yaliyosalia ya ulinzi katika muda mwafaka. 

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ameeleza kuwa, amekuwa na mazungumzo mazuri hapa Tehran na kwamba wanatekeleza majukumu yao na wanasubiri kurejea kikamilifu katika mapatano. Amesema kinachohitajika ili kukamilisha mazungumzo ya nyuklia ya Iran huko Vienna ni ushirikiano.