Saudia ibebe lawama za kushindwa Wairani kwenda Hija mwaka huu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i8167-saudia_ibebe_lawama_za_kushindwa_wairani_kwenda_hija_mwaka_huu
Mkuu wa Idara ya Ghuba ya Uajemi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, ukoo tawala wa Aal Saud wa Saudi Arabia ndio unaopaswa kubeba lawama za kushindwa Waislamu wa Iran kwenda Hija mwaka huu.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
May 31, 2016 07:46 UTC
  • Saudia ibebe lawama za kushindwa Wairani kwenda Hija mwaka huu

Mkuu wa Idara ya Ghuba ya Uajemi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, ukoo tawala wa Aal Saud wa Saudi Arabia ndio unaopaswa kubeba lawama za kushindwa Waislamu wa Iran kwenda Hija mwaka huu.

Mohammad Omrani amesema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na toleo la leo la gazeti la Itimad la mjini Tehran kwamba kutokana na kwamba haram mbili tukufu ziko katika ardhi ya Saudia, na ukoo wa Aal Saud ndio ulioko madarakani nchini humo, viongozi wa nchi hiyo ndio wanaobeba jukumu la kila jambo linalotokea kuhusiana na ibada ya Hija. Amesema, siasa za hivi sasa za utawala Aal Saud hazikubaliki kabisa, na nchi za Kiislamu haziwezi kukubaliana na suala hilo. Ikumbukwe kuwa, Saudi Arabia imewawekea masharti magumu sana Waislamu wa Iran, jambo ambalo linawawia vigumu Waislamu wa Iran kwenda Hija mwaka huu. Kwa mujibu wa Mkuu wa Shirika la Hija na Ziara la Iran Saeed Ohadi, sababu ambazo zimepelekea Mahujaji wa Iran washindwe kutekeleza ibada ya Hija mwaka huu ni kitendo cha Saudia kupiga marufuku marufuku kuwekwa bendera ya Iran katika majengo ya Mahujaji wa Iran, kuweka vizingiti kuhusu idadi ya zahanati za Iran katika msimu wa Hija kukataa mahujaji wa Iran kuvaa utepe wa kielektroniki wa kuwatambulisha Mahujaji wa Iran, kupiga marufuku baadhi ya hafla za Mahujaji wa Kiirani na pia dharau kubwa zinazooneshwa na maafisa wa Saudia kuhusiana na nakala za Qur'ani Tukufu zinazochapishwa nchini Iran.