Rais Maduro wa Venezuela aitembelea Iran kwa ziara ya siku 2
(last modified Sat, 11 Jun 2022 02:40:39 GMT )
Jun 11, 2022 02:40 UTC
  • Rais Maduro wa Venezuela aitembelea Iran kwa ziara ya siku 2

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela aliwasili hapa Tehran jana Ijumaa kwa safari rasmi ya kikazi ya siku mbili ya kuitembelea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Hayo yameripotiwa na shirika la habari la IRNA ambalo limeeleza kuwa, Rais Maduro anaongoza ujumbe wa ngazi ya juu wa kisiasa na kiuchumi wa nchi hiyo katika ziara hiyo hapa nchini.

Rais wa Venezuela anatazamiwa kukutana na kufanya mazungumzo na maafisa wa ngazi za juu wa Iran, akiwemo mwenyeji wake aliyemualika Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu.

Uhusiano wa pande mbili wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Venezuela umekuwa ukiimarika siku baada ya siku, haswa kwa kuzingatia kuwa mataifa haya mawili yana mambo mengi yanayoyakurubisha pamoja.

Rais Raisi wa Iran (kulia) na Maduro wa Venezuela

Mataifa haya mawili kwa miaka mingi sasa yamekuwa wahanga wa mashinikizo na vita vya kiuchumi vya Marekani, kutokana na kusimama kwao kidete kupinga sera za kibeberu za Washington.

Licha ya kuendelea mashinikizo ya kisiasa na kiuchumi ya Marekani dhidi ya taifa na serikali ya Venezuela, lakini taifa hilo la Amerika ya Latini limesimama kidete dhidi ya ubeberu na limefanikiwa kuibuka na ushindi.

Tags