Nchi za Kiislamu zibadili usimamizi wa Hija
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i8542-nchi_za_kiislamu_zibadili_usimamizi_wa_hija
Mkuu wa Shirika la Hija na Ziara za Kidini la Iran amesema kuna udharura wa nchi za Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu kuanzisha mkakati wa kubadilisha muundo wa usimamizi wa Ibada ya Hija na kuzuia mwenendo wa ubaguzi na utumiaji mabavu wa Saudi Arabia kuhusu ibada hiyo ya kila mwaka.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 06, 2016 03:49 UTC
  • Nchi za Kiislamu zibadili usimamizi wa Hija

Mkuu wa Shirika la Hija na Ziara za Kidini la Iran amesema kuna udharura wa nchi za Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu kuanzisha mkakati wa kubadilisha muundo wa usimamizi wa Ibada ya Hija na kuzuia mwenendo wa ubaguzi na utumiaji mabavu wa Saudi Arabia kuhusu ibada hiyo ya kila mwaka.

Saeed Ouhadi Mkuu wa Shirika la Hija la Iran katika mazungumzo na mwandishi wa Radio Tehran amesema: "Kubadilisha muundo wa usimamizi wa Hija ni suala muhimu kwa nchi za Kiislamu. Hii ni kwa sababu nchini nyingi zimeshuhudia muamala mbovu wa maafisa wa Saudia katika msimu wa Hija."

Ouhadi amebainisha kuwa Masjidul Haram mjini Makka na Masjid Nabawi mjini Madina ni milki za Waislamu wote duniani.

Ameongeza kuwa, maafisa wa utawala wa Saudia huamiliana vibaya na mahujaji Wairani jambo ambalo limewakera maulamaa. Amesema Wasaudia wamewazuia Wairani kuhiji mwaka kuu hutokana na sisitizo la Iran la kuheshimiwa wageni wa Mwenyezi Mungu.

Mkuu wa Shirika la Hija la Iran amesema watawala wa Saudia wamewazuia Wairani kuhiji mwaka huu na hivyo wao ndio watakaobeba lawama zote za ubaguzi huo.

Ouhadi pia amekosoa Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudia kwa kupuuza hotuba za kichochezi za wahubiri mjini Makka ambao wamehalalisha kumwagwa damu ya Waislamu wa madhehebu ya Shia. Aidha amekosoa hatua ya watawala wa Saudia ya kuingiza masuala yao binafsi ya kisiasa katika Ibada ya Hija.