Marekani inaendeleza uhasama dhidi ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i8716-marekani_inaendeleza_uhasama_dhidi_ya_iran
Naibu Waziri wa Uchumi wa Iran amesema msingi wa sera za serikali ya Marekani ni kuendeleza sera za uhasama dhidi ya Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 07, 2016 10:00 UTC
  • Marekani inaendeleza uhasama dhidi ya Iran

Naibu Waziri wa Uchumi wa Iran amesema msingi wa sera za serikali ya Marekani ni kuendeleza sera za uhasama dhidi ya Iran.

Mohammad Khazaee katika mahojiano na Shirika la Habari la Mehr amesema, haiwezekani kutegemea Marekani isikitishwe na vitendo vyake dhidi ya Iran au iombe radhi kwani dhati ya sera zake haiiruhusu kufanya hivyo.

Khazaee amesema vikwazo vya kimataifa dhidi ya Iran vimeporomoka lakini watawala wa Marekani wanaendeleza vitendo vyao vya chuki dhidi ya Iran.

Khazaee amesema kuwa, Russia, China na India zilikuwa na uhusiano mzuri na Iran hata wakati nchi hii ilipokuwa imewekewa vikwazo na kwa msingi huo nchi hizo mbili zinapewa kipaumbele na Iran katika ushirikiano wa kiuchumi.

Itakumbukwa kuwa, Julai 14 mwaka uliopita, Iran ilifikia makubaliano ya kihistoria na nchi za Marekani, Uingereza, Ufaransa, Uchina, Russia pamoja na Ujerumani ambazo zinaunda kundi la 5+1 kuhusiana na miradi yake ya nyuklia. Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Iran imetakiwa kupunguza baadhi ya mambo kwenye miradi yake ya nyuklia mkabala wa kuondolewa vikwazo vya kimataifa. Tayari utekelezwaji wa makubaliano hayo umeanza na vikwazo vya kimataifa dhidi ya Iran vimeondolewa.