Kanani: Iran inaunga mkono kuendelezwa mchakato wa kusitisha mapigano huko Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i88100-kanani_iran_inaunga_mkono_kuendelezwa_mchakato_wa_kusitisha_mapigano_huko_yemen
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa Iran inaunga mkono kuendelezwa na kuimarishwa mchakato wa kusitisha mapigano nchini Yemen.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 12, 2022 22:02 UTC
  • Kanani: Iran inaunga mkono kuendelezwa mchakato wa kusitisha mapigano huko Yemen

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa Iran inaunga mkono kuendelezwa na kuimarishwa mchakato wa kusitisha mapigano nchini Yemen.

Nasser Kanani ameashiria matukio ya karibuni na kueleza kuwa: Iran inaafiki kuendelezwa na kuimarishwa mwenendo wa usitishaji vita huko Yemen na kwamba  kinachoweza kusaidia kuimarika kwa mwenendo huo wa usitishaji vita ni kuondoa mzingiro na kuwadhaminia mahitaji yao wananchi wa Yemen walio chini ya mzingiro.  

Kuhusu matukio ya karibuni huko Afghanistan, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran pia ameeleza kuwa: Jamhuri ya Kiislamu siku zote imekuwa ikipokea idadi kubwa ya wakimbizi wa Kiafghani na kwa miaka kadhaa sasa Iran ni mwenyeji wa mamilioni ya wakimbizi wa nchi hiyo. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa: Iran ipo tayari kufanya mazungumzo na nchi jirani na rafiki katika ukanda huu; hiyo utekelezaji wa sera zisizofaa katika mkondo wa mazungumzo hausaidii lolote. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran pia amezungumzia Mkutano wa Shanghai huko Samarkand na uanachama wa kudumu wa Iran katika jumuiya hiyo na kusema: Hatua za kiutendaji zimechukuliwa kwa ajili ya uanachama wa Iran katika jumuiya hiyo.

Mkutano wa Jumuiya ya Shanghai, Samarkand 

Kanani ameongeza kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ikiwa ni nchi muhimu katika eneo la Magharibi mwa Asia, ina rasilimali muhimu za nishati na uwezo wa kiuchumi na  kutokkana na kuwepo kwake katika njia ya korido ya kaskazini-kusini, Iran inaweza kwenda sambamba na  malengo muhimu ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai.