Saudia inaunga mkono ugaidi na kuua watu wasio na hatia Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i8893-saudia_inaunga_mkono_ugaidi_na_kuua_watu_wasio_na_hatia_yemen
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran amesema: Jinai za utawala wa Saudia dhidi ya watu wasio na hatia Yemen na uungaji mkono wake kwa ugaidi katika eneo ni mambo yanayofanyika kwa mashali ya madola ya kiistikbari na Uzayuni wa kimataifa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 10, 2016 09:33 UTC
  • Saudia inaunga mkono ugaidi na kuua watu wasio na hatia Yemen

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran amesema: Jinai za utawala wa Saudia dhidi ya watu wasio na hatia Yemen na uungaji mkono wake kwa ugaidi katika eneo ni mambo yanayofanyika kwa mashali ya madola ya kiistikbari na Uzayuni wa kimataifa.

Ayatullah Mohammad Ali Muwahidi Kermani katika hotuba za Sala ya Ijumaa mjini Tehran amebainisha masikitiko yake kuhusu hatua ya utawala wa Aal Saud kuendeleza vita na kumwaga damu ya watu wa Yemen. Amesema kuuawa wanawake na watoto wa Yemen ni mfano wa wazi wa mauaji ya kimbari.

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya mjini Tehran amebainisha kuwa, Saudi Arabia inatoa uungaji mkono wa kifedha na kilojistiki kwa makundi ya kigaidi katika eneo na kwamba ukoo wa Aal Saud unafanya kila uwezalo kufanikisha sera chafu za Marekani na Utawala wa Kizayuni katika eneo.

Ayatullah Kermani ameendelea kusema kuwa, sera za Saudia za uhasama dhidi ya nchi za Kiislamu katika eneo zinajiri wakati ambao nchi hiyo inadai eti ni "Khadimul Haramein" au mhudumu wa maeneo mawili matakatifu ya Makka na Madina. Amesema kuendelea sera kama hizo hakutakuwa na natija nyingine isipokuwa kuangamia utawala wa Aal Saud.

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran pia ameashiria kustawi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika sekta mbali mbali na kusema, wakuu wa mihimili mitatu ya dola wanapaswa kushirikiana katika kuondoa matatizo na vizingiti katika njia ya ustawi zaidi wa Iran. Aidha ametoa wito kwa wananchi na wakuu serikalini kutohadaiwa na adui na wawe waaangalifu kuhusu njama za Marekani dhidi ya Iran katika sera za utamaduni, siasa na uchumi.