Mkutano wa 36 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu kufanyika Tehran
(last modified Sun, 09 Oct 2022 14:25:48 GMT )
Oct 09, 2022 14:25 UTC
  • Mkutano wa 36 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu kufanyika Tehran

Mkutano wa 36 wa kimataifa wa Umoja wa Kiislamu unatarajiwa kufanyika wiki ijayo hapa jijini Tehran kwa kuhudhuriwa na makumi ya shakhsia wa kidini wa ndani na nje ya nchi kwa mnasaba wa maadhimisho ya Wiki ya Umoja.

Katibu Mkuu wa Baraza la Kimataifa la Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu amesema kuwa, Mkutano wa 36 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu utafunguliwa wiki hii kwa hotuba ya Rais Ibrahim Raisi wa Jamhurii ya Kislamu ya Iran.

Hujjatul Islam Hamid Shahriyari, Katibu Mkuu wa Baraza la Kimataifa la Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu amesema kuwa, mkutano huo unatarajiwa kufanyika kuanzia Jumatano hadi Ijumaa za wiki ijayo.

Kwa mujibu wa  Katibu Mkuu wa Baraza la Kimataifa la Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu ni kuwa, mkutano huo utakaofanyika hapa mjini Tehran unatarajiwa kuhudhuiwa na zaidi ya shakhsia 300 wa ndani na kutoka mataifa ya kigeni.

Hujjatul Islam Hamid Shahriyari, Katibu Mkuu wa Baraza la Kimataifa la Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu

 

Mkutano wa mara hii unafanyika chini ya nara na kaulimbiu ya "Umoja wa Kiislamu, amani, kujiiepusha na mifarakazo na mizozo katika Ulimwengu wa Kiislamu.

Aidha Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu anatarajiwa kukutana na washiriki wa mkutano huo wa kimataifa wa Umoja wa Kiislamu baada ya kukamilisha mkutano wao siku ya Ijumaa.

Mkutano wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu hufanyika kila mwaka kwa mnasaba wa Wiki ya Umoja wa Kiislamu.

Ni vyema kuashiria hapa kuwa, Wiki ya Umoja wa Kiislamu ni kipindi cha kati ya tarehe 12 na 17 za Mfunguo Sita Rabiu Awwal kipindi ambacho kinasadifiana na kuadhimisha Maulidi na kumbukumbu ya kuzaliwa Bwana Mtume SAW.