Iran: Ulaya italipa gharama kubwa kwa hatua zake dhidi ya IRGC
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i93272-iran_ulaya_italipa_gharama_kubwa_kwa_hatua_zake_dhidi_ya_irgc
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema uingiliaji kati wa Bunge la Ulaya, na hatua ya kihisia ya taasisi hiyo ya kupiga kura ya kuliongeza Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) katika orodha ya eti makundi ya 'kigaidi' ya Umoja wa Ulaya itakuwa na matokeo mabaya, na kwamba Ulaya italipa gharama kubwa kwa hatua zake hizo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 24, 2023 23:34 UTC
  • Iran: Ulaya italipa gharama kubwa kwa hatua zake dhidi ya IRGC

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema uingiliaji kati wa Bunge la Ulaya, na hatua ya kihisia ya taasisi hiyo ya kupiga kura ya kuliongeza Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) katika orodha ya eti makundi ya 'kigaidi' ya Umoja wa Ulaya itakuwa na matokeo mabaya, na kwamba Ulaya italipa gharama kubwa kwa hatua zake hizo.

Hossein Amir-Abdollahian alisema hayo jana Jumanne akihutubia mkutano wa 26 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya ECO katika mji wa Tashkent, Uzbekistan. 

Amir-Abdollahian amesisitiza katika hotuba yake hiyo kuwa, "Hakuna shaka, matokeo mabaya ya hatua hiyo ya kihisia ya Ulaya itaigharimu yenyewe pakubwa."

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran  amebainisha kuwa, sera za nje za Jamhuri ya Kiislamu zimejengwa katika msingi wa maingiliano yenye mlingano na dunia, na kutoingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine. 

Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Iran amekariri kuwa, hatua hiyo ghalati ya Ulaya haitapita bila kujibiwa, na kwamba Bunge la Iran linajiandaa kuviweka vitengo vya majeshi ya nchi za Ulaya kwenye orodha ya magaidi.

Wanajeshi wa SEPAH

Bunge la Umoja wa Ulaya Jumatano iliyopita lilipitisha marekebisho ambayo yaliongezwa kwenye ripoti ya kila mwaka ya sera ya mambo ya nje na kutaka nchi wanachama wake kujumuisha IRGC katika orodha yao ya magaidi.

Aidha Ulaya imepasisha vikwazo zaidi dhidi ya watu binafsi na mashirika ya Iran, sanjari na kuiweka IRGC katika orodha ya magaidi wa Umoja wa Ulaya, eti kutokana na madai ya ukiukaji wa haki za binadamu wakati wa ghasia za hivi majuzi.